Breaking News

Your Ad Spot

Mar 20, 2012

SAU:BILA KUSHIKAMA NI NDOTO WAPINZANI KUSIHINDA CCM KATIKA UCHAGUZI

Shabani Kirita wa SAU
Meru
Chama Cha Sauti ya Umma (SAU) kimesema vyama vya upinzani hapa nchini vimekuwa vikishindwa na CCM katika uchaguzi mbalimbali kwa  sababu ya ubinafsi.


Hayo yalisemwa leo na mgombea ubunge jimbo la Arumeru Mashariki kwa tiketi ya chama hicho, Shabani Kirita wakati akihutubia wananchi katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni zake uliofanyika Majani ya Chai.


Alisema, njia madhubuti ambayo ingewezesha upinzani kuishinda CCM ni kwa vyama vya upinzani kuwa na kuungana, lakini akasema hilo limekuwa likishindikana kila unapotokea uchaguzi kutokana na uroho wa viongozi katika vyama hivyo hasa vyenye ruzuku.


Kirita alivitaja vyama vye kupata ruzuku kuwa ni pamoja na CUF, CHADEMA, UDP, NCCR Mageuzi na TLP, na kwamba viomgozi wa vyama hivyo ni walafi wa kupindukia ndiyo sababu hakuna hata mmoja kati yao anayefikiria kuwa ni muhimu vyama vya upinzani kuungana dhidi ya CCM.


"Sisi SAU tunasema kwamba tuna miaka michache katika ulingo wa siasa hapa nchini, lakini 'tunatisha' na kwa sababu tunaamini kwamba tupo kwa ajili ya kuinua maisha ya wananchi kwa kutumia sauti ya umma tupeni nafasi ya ubunge hapa Arumeru tuonyeshe mfano", alisema.


Alisema, wakati baadhi ya vyama vinajinadi kuwa ni 'Nguvu ya Umma' faida ya nguvu hiyo imekuwa ikiwanufaisha viongozi wa vyama hivyo wakati umma unaowaunga mkono ukiendelea kudorora kimaisha.


Kwa upande wake Meneja wa kampeni wa mgombea huyo, Johnson Mwangosi aliwataka wana Arumeru Mashariki, kuchagua mgombea mwenye sifa zitakazowanufaisha wote, na siyo kwa  kulazimishwa au kutishwa na viongozi wa vyama vya wagombea.


Aliwataka vijana kujiepusha kutumiwa na viongozi wa vyama vya siasa vyenye wagombea kama chambo cha kuwa mstari wa mbele kwenye vurugu kwa manufaa ya viongozi hao.


"vijana jihadharini sana, msitumbukie katika vujo na vurugu wakati wa kampeni na kwenye uchaguzi wenyewe kwa sababu eti umepewa bia mbili, ukiingia katika mtengo huo ukiumia, kufa au kukamatwa utakuwa peke yako", alisema.


Kampeni za uchaguzi mdogo jimbo la Arumeru mashariki zilianza kurindima tangu Machi tisa mwaka huu, na zitatia nanga Machi 31, mwaka huu kupisha uchaguzi utakaofanyika Aprili Mosi mwaka huu.

1 comment:

  1. Добрый день! Нашел отличную возможность сделать БЕСПЛАТНО сайт для компании

    Можно создать для себя интернет-магазин или корпоративный сайт - за 30 минут. Эта система очень простая, разберется любой!

    Если интересно, можно заглянуть в группу http://vk.com/neosite или зайти на офф. сайт: http://demo.neobroker.ru

    ReplyDelete

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages