Breaking News

Your Ad Spot

Apr 7, 2012

BASATA WAMLILIA KANUMBA

MASIKITIKIO JUU YA KIFO CHA MSANII STEVEN CHARLES KANUMBA
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limepokea kwa masikitiko na majonzi makubwa taarifa ya kifo cha Msanii wa filamu Steven Charles Kanumba kilichotokea usiku wa kuamkia leo Jumamosi ya Tarehe 07/04/2012 baada ya kuanguka ghafla akiwa nyumbani kwake Sinza Vatican jijini Dar es Salaam.
   BASATA inaungana na familia za wafiwa na wasanii wote nchini kwa maombolezo  ya msiba huu mkubwa na wa kihistoria.  Kufiwa na msanii huyu mahili kwenye tasnia ya filamu ni pengo kubwa kwa familia, Sekta ya sanaa na Taifa kwa ujumla kutokana na ukweli kuwa, aliweza kuutangaza utamaduni na sanaa yetu nje ya mipaka.
    Kanumba atakumbukwa kwa moyo wake wa kujituma na kuthamini kazi ya Sanaa toka akiwa Kundi la Maigizo la Kaole ambapo moyo wake huo ulimfanya awe miongoni mwa wasanii walioleta mageuzi kwenye tasnia ya filamu kwa kuifanya kuanza kupendwa na wadau wengi zaidi.
    Aidha, atakumbukwa kwa juhudi zake za kuinua vipaji vichanga katika tasnia ya filamu ambapo mara kadhaa katika kazi alizoziandaa alishirikisha wasanii wachanga ambao BASATA inaamini watakuja kuwa hazina kubwa kwa taifa letu.
     BASATA linatoa pole kwa familia ya marehemu na Wasanii wote katika kipindi hiki kigumu. Ni vema wasanii wote tukatumia kipindi hiki kutathimini kwa pamoja michango yetu katika kukuza sekta ya Sanaa ikiwa ni pamoja na kuimarisha umoja wetu lakini pia tukiyaenzi yale yote mema yaliyofanywa na Steven Charles Kanumba.
     Mungu ailaze roho ya Marehemu Steven Charles Kanumba mahali pema peponi. AMEN
      Sanaa ni Kazi Kwa Pamoja Tuikuze na Kuithamini.
Ghonche Materego
KATIBU MTENDAJI, BASATA

Barua zote ziandikwe kwa Katibu Mtendaji
All correspondence to be addressed to The Executive Secretary
BASATA Arts Centre, Ilala Sharif Shamba, P.O. Box. 4779, Dar es Salaam, Tanzania.
Telephone: 2863748/2860485, Fax: 0255 - (022) - 286 0486 E-mail: info@basata.or.tz Website: basata.or.tz

2 comments:

  1. ATAKAE TANGAZA NIA SHINYANGA MJINI KUKIONA.---KANUMBA AMEKIPATA................
    Habari imeeleza kuwa yeyote atakaye tangaza kugombea ubunge jimbo la shinyanga mjini hatari ipo mbele yake, hii inatokana na mmliki wa Jimbo hilo Mh steiven Masele kujipanga kuhakikisha ana wamaliza wabaya wake wote kwa ndumba.

    Alianza na Shelembi mtu ambaye si tu kwamba alipendwa sana mjini Shinyanga pia ndiye aliyeshinda ubunge wa hilo jimbo mwaka 2010 lakini hakutangazwa, baada ya muda mfupi alifariki dunia na tetesi zinasema aliuwawa na mganga wa Steiven Masele ambaye anaishi huko Mwamadulu ambaye ni mama yake na mbunge huyo kijana anayeendekeza sana ushirikiana. Kifo cha Shelembi kimetokea karibuni mwaka mmoja sasa umepita na CHADEMA mkoa wa shinyanga wako kwenye maandalizi ya kumbukumbu yake.

    Muda si mrefu Kanumba alichukua kadi ya chama cha demokrasia na maendeleo kwa msaada mkubwa wa mwenyekiti wa BAVICHA John Heche, ana Heche alikuwa anampigia chapuo kwa viongozi wa chadema taifa ili awe mgombea wake kwenye uchaguzi mkuu wa 2015 kwa ngazi ya ubunge mjini Shinyanga.

    Mtoa habari hizi amedai kuwa baada ya bwana masele kugundua kuwa popularity ya bwana kanumba ni kubwa njia pekee ni kumuondoa duniani, wengine wanaotajwa kwa majina kuwa wako kwenye orodha ya kutangulia mbele ya haki kama tu watatangaza nia au watajaribu kugombea jimboni humu wameonywa, ndugu Tumbo ambaye siku za karibuni amekuwa akipigana kumbo na viongozi wa mkoa hapa shinyanga kwa lengo la kugombea uenyekiti wa mkoa ili baadaye aje ajiteuwe kuwa mgombea wa ubunge wa jimbo hilo.

    Mwingeine ni Rachel mashishanga ambaye ni mbunge wa viti maalum amabye naye kwa kutumia wapambe wake amekuwa akuhusishwana hizo tetesi za kutaka kugombea na aliwahi kusikika katika mkutano wa kampeni kata ya masekelo akiwasihi wananchi wamchague diwani wa Chadema ili wampe moyo wa yeye kugombea hilo Jimbo, mara tu baada ya kauli yake hiyo siku mbili baadaye alianza kuumwa miguu kiasi amabcho alishindwa hata kutembea na sidhani kama bado ana hiyo nia.

    Vijana wengine wa Shinyanga pia wameshatangaza hizo nia wengine kupitia mitandao ya kijamii, kuna huyu mmliki wa forum ya shinyanga tunayoitaka ameshatangaza kuwa atagombea kupitia ccm lakini hana madhara kwa ndugu masele ndiyo maana bado anaishi, Huo ni muendelezo wa siasa za kichawi kanda ya ziwa.

    Ikumbukwe kuwa jimbo la solwa ambalo ni jimbo jirani na shinyanga mjini mwaka 2000-2004 liliwahi kuuwa wabunge wanne na dawa hiyo nasikia ndiyo iliyohamia mjini shinyanga kilimalizia chanzo cha taarifa hiyo- HUU NI UKWELI ATUNA MUDA WA KUSEMA UONGO ILI USAIDIE NINI?

    ReplyDelete
  2. ATAKAE TANGAZA NIA SHINYANGA MJINI KUKIONA.---KANUMBA AMEKIPATA................

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages