Breaking News

Your Ad Spot

Apr 5, 2012

GODBLESS LEMA AVULIWA UBUNGE ARUSHA

Aliyekuwa mbunge wa Arusha mjini, Lema
Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imemvua ubunge, aliyekuwa mbunge wa jimbo la Arusha mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Godbless Lema.
         Mahakama hiyo imetoa uamuazi huo katika kesi iliyokuwa inamkabili Lema ya kupinga matokeo yaliyompa ubunge Lema baada ya  uchaguzi mkuu wa mwaka 2010
         Katika kesi hiyo iliyofunguliwa na wapigakura watatu, Mussa Mkanga,  Happy Kivuyo na Agnes Mollel  ilimlalamikia Lema kuwa alitoa matamshi ya matusi na kejeli dhidi ya aliyekuwa mgombea wa CCM, Dk. Matilda Salha Burian.
         Hukumu imetolewa leo  na Jaji  Gabriel Rwakibarila wa Sumbawanga, huku umati wa watu ukisubiri kwa shauku za namna mbalimbali.
         Kwa mujibu wa habari kutoka Arusha, baada ya hukumu hiyo, Lema amesema fursa ya kukata rufani aliyopewa na mahakama hiyo, hataitumia badala yake, anasubiri kuingia tena kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi Tume ya Taifa ya Uchaguzi itakapopiga kipyenga.
Lema amesema, uamuzi wa mahakama amekubaliana nao, na kilichobaki anasubiri uamuzi wa wananchi wenyewe wa Arusha, badala ya kutaka awe mbunge wa mahakamani.
          Wakati Lema akisema hivyo, Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe yeye amesema uamuzi wa kukata rufani au kusubiri kujitosa katika uchaguzi utatolewa na chama hicho keshokutwa Jumanosi.
UCHUNGU WA KUSHINDWA! Wafuasi wa Chadema wakiwa taabani kiasi cha wengine kulia kama mama huyu,  baada ya kusikia hukumu hiyo dhidi ya  Lema. Wafuasi  hao wa Chadema walikuwa ndani ya viwanja vya mahakama kuu kanda ya Arusha wakati hukumu ikitolewa na kumuona Lema ana hatia na hivyo kuvuliwa ubunge na Jaji

WALIMLIZA LEMA: Wapiga kura watatu waliofungua kesi ya kupinga matokeo ya ubunge dhidi ya  Lema wakiwa mahakamani kabla ya hukumu ya kesi hiyo kuanza kusomwa na jaji Gabriel Rwakibarila katika mahakama kuu kanda ya Arusha, Kushoto ni  Mussa Mkanga,  Happy Kivuyo na Agnes Mollel (Picha zote kwa hisani ya  Shaaban Mdoe wa gazeti la Uhuru).

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages