.

CHADEMA WAFUKUZANA KIGOMA

Apr 23, 2012


CHADEMA wametangaza kumfukuza uanachama Mwenyekiti wa jimbo la Kigoma Kusini, Jumanne Bilango kwa tuhuma za kukiuka maadili ya uongozi.


Hatua hiyo imetangazwa na Katibu wa chama hicho jimboni humo, Shaban Madede, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye soko la Kazuramimba na kueleza kuwakamati ya sektretarieti ya jimbo imeridhia uamuzi uliochukuliwa na tawi la CHADEMA la Kazuramimba kumvua uanachama Mwenyekiti huyo.


Madede alisema tuhuma kubwa dhidi ya Mwenyekiti huyo inaelezwa kuwa alishindwa kuwasilisha sh. 250,000 zilizotolewa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe mwaka 2004 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa shule ya sekondari ya kata hiyo.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช