James Ole Millya |
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) mkoa wa Arusha James Ole Millya ambaye ameshajipeleka Chadema amedaiwa kusepa na sh. milioni 2 alizokabidhiwa kwa ajili ya kuanzisha SACCOS ya UVCCM mkoani humo.
Habari zinasema, bunda hilo la sh. milioni 2 zilitolewa na Felix Mrema aliyekua mbunge wa Arusha mjini na Elisa Mollel aliyekua mbunge wa Arumeru Magharibi, walitoa hundi ya Sh.milioni 1 kila mmoja, Desemba 2008, katika Baraza la kwanza la Vijana lililofanyika Karatu.
Akizungumza na mtandao huu, Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM mkoani Arusha, Mrisho Gambo amemtaka Millya kurudisha fedha hizo haraka ili ziendeleze shughuli ya kuanzisha SACCOS mkoani hapa, kwa lengo la kujenga uchumi wa Vijana.
Aidha ametoa angalizo kwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe kumwangalia Millya ambaye ni mroho wa madaraka na mchochezi wa vurugu na kuwa,hata kama anataka kumudu mabadiliko ndani ya chama kipya, wampe nafasi moja tu Wilayani Monduli, waone kama atafanya kazi au majungu.
Gambo alisema kwanza wamefurahi Millya kuhamia Chadema,kwani alikuwa ni mtu anayesababisha pancha kwenye tairi,lenye gari kubwa na tangu Millya alipochaguliwa kuwa mwenyekiti hakuwahi kufanya Maendeleo yoyote ndani ya UVCCM,wala kuleta tija, bali alikuwa ni kiongozi mwenye kuleta migogoro na maandamano, kila kukicha ndani ya chama pamoja na kutetea mafisadi.
Alisema Millya anasumbuliwa na uroho wa madaraka akitoa mfano alitaja mwaka 2010 aligombea nafasi na Mbunge wa Simanjiro,Christopher Ole Sendeka,akashindwa na umri wake pia umepita kugombea tena nafasi ya UVCCM, ndio maana akaona bora akijiengue, kwani hana nafasi tena ya kugombea ndani ya CCM na kwakuwa alikosa nafasi ya kugombea Ubunge wa Afrika Mashariki,akaona hapa ni pagumu na kuhamia Chadema.
Millya ameamua kufanya siasa ili apate kipato kwasababu ni kibaraka wa mafisadi na kuongoza msafara wa magamba dagaa, huku magamba makubwa yakijiandaa kuondoka.
“Tunamtaka atukabidhi ofisi na kulipa deni letu la Sh.milioni 2 zilizotolewa kwa ajili ya kuanzisha SACCOS na ameingiza hasara chama zaidi ya milioni 600,hivyo tunasema Millya ni msumari uliokuwa ukisababisha pancha, kila mara na kila wakijitahidi kuliondoa gari hilo,lilikuwa linawekwa kiraka na mafisadi, hivyo ni bora aliyekuwa akisababisha pancha kaondoka mwenyewe,”alisema.
Alisema kuwa kuhusu kauli kuwa amekosa nafasi ya Ubunge Afrika Mashariki na kumweka Gambo ambaye hana sifa kama zake,alisema kuwa sio kweli kwa sababu wote walikuwa na onyo ndani ya chama na wana digrii mbili, ila tofauti zao ni sifa ambazo yeye ni Mwenyekiti wa Asasi ya Vijana Afrika Mashariki na Mchambuzi wa Mifumo ya Kompyuta Manispaa ya Arusha, tofauti na Millya hajulikani kazi yake wala anapoishi.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269