Magesa Milongo |
MKUU wa mkoa wa Arusha Bw Magesa Mulongo amevunja ukimya na kusema kuwa wawekezaji ambao wapo kwenye shamba la Doll Estate ambalo wananchi waliwavamia wawekezaji hao wiki chache zilozipita kuwa wawekezaji hao wapo sawa kisheria.
Bw Mulongo alisema hayo jana wakati akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari ambapo alidai kuwa kuvamiwa kwa wawekezaji hao katika shamba la Doll kuna mkono wa kisiasa ambao unawapa nguvu za vurugu kwa baadhi ya wananchi.
Alifafanua kuwa pamoja na kuwa shamba hilo ambalo wananchi wanadai kuwa ni mali yao uongozi wa mkoa ulifanya jitiada mbalimbali za kuhakikisha kuwa zinarudiaha amani katika eneo hilo ambalo Wananchi
waliwavamia wawekezaji hao na kisha kuharibu mali.
“pamoja na kuwa tulijaribu kufanya kila jitiada ya kuhakikisha kuwa kunakuwa na maelewano lakini bado wananchi hao walirudi tena na kuvamia shamba hilo kwa nia ya kuharibu mali za wawekezaji hao ambao
wapo sawa kwa mujibu wa sheria “aliongeza Mkuu huyo wa Mkoa
Katika hatua nyingine alisema kuwa Madai ya Ardhi ambayo yanaendelea kukua na kuibuka hasa kwa wananchi kujaribu kuwavamia wawekezaji ndani ya Wilaya hiyo ya Arumeru wananchi wanapswa kujua na kufuata taratibu
mbalimbali kama kweli nia yao ni kupata ardhi ambayo wanaitaka kwa mujibu wa Sheria na Taratibu za Nchi
Aliongeza kuwa vitendo hivyo vya vurugu ambavyo vinafanywa na baadhi ya wananchi ambao wanadai kuwa Ardhi ni mali yao vinasababisha sana uharibifu wa mali za wawekezaji hao jambo ambalo ni hatari sana hata kwa maslahi ya Taifa.
“kutokana na kuendelea kukithiri sana kwa vitendo hivi vya ardhi ndani ya wilaya hiyo ninachosema kuwa Kamwe Jeshi la Polisi halitasita kuchukua hatua kwa mwananchi yeyote yule ambaye atahusika na uchochezi,pamoja na uvunjwaji wa sheria za nchi”alisema Bw Mulongo
Mbali na hayo mkuu huyo alisema kuwa mpaka sasa wamefanikiwa kugundua kuwa wapo baadhi ya wanasiasa ambao ndani ya jimbo hilo ambao wanatumia fursa hiyo kwa kuhamasiasha wananchi kufanya vurugu kinyume cha sheria na taratibu za Nchi ya Tanzania hivyo wakibainika watachukuliwa hatua dhidi yao kwa kuwa ndio wanahamasisha wananchi kufanya vurugu hizo.
“kama kuna mtu yeyote ambaye amewahidi wananchi kuwa atawapa ardhi ya wawekezaji hao ni vema basi wananchi wakamfuata ili aweze kuwapa ardhi lakini pia mtu huyo anatakiwa kwanza kuijua sheria kabla ya
kuwasihi wananchi waweze kuharibu mali za watu”alisema Bw Mulongo
Katika hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa aliwataka wawekezaji na wamiliki wa mashamba hayo kuhakikisha kuwa wanatekeleza vema wajibu wao kwa wananchi wanaowazunguka ikiwa ni pamoja na kusaidia kupatikana
kwa huduma za msingi za kijamii , ambapo kwa Wawekezaji wa mashamba hayo wanafanya kikamilifu.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269