.

UWT TAWI LA MAKAO MAKUU YA CCM LUMUMBA WAPATA VIONGOZI WAPYAAAA

Apr 24, 2012

Mary Nchimbi
 Umoja Wanawake wa CCM, Tawi la Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, umefanya uchaguzi na kupata viongozi wapya.


Katika uchaguzi huo, Mary Nchimbi ameibuka kuwa Mwenyekiti wa mpya wa tawi hilo baada ya kupata kura 34 dhidi ya kura 28 alizopata mpinzani wake Sheila Luckusasi.


Nafasi ya Katibu wa tawi hilo ilikwenda kwa Naomi Daudi ambaye alijizolea kura 62 na kumwacha mbali mpinzani wake, Arafa Athumani aliyeambulia kura mbili tu.


Katika nafasi ya Ujumbe wa kuwakilisha Tawi kwenye ngazi ya wilaya ulikwenda kwa Sheila Luckusasi ambaye baada ya kukosa Uenyekiti alifuta machozi kwa kupata nafasi hiyo kwa taabu baada ya kumshinda mpinzani wake Zainab Bwamkuu kwa kura moja kwa kupata kura 36 dhidi ya 35.


Pia Selina Mbelwa naye aliibuka mshindi katika kinyang'anyiro cha ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Tawi baada ya kujipatia kura 40 dhidi ya 30 alizopata mpinzani wake Jeni Mafinga.
 Mary akipongezwa na mgombea mwenzake wa Uenyekiti Sheila Luckisasi baada ya matokeo
 Wajumbe wakiwa kwenye mkutano huo wa uchaguzi kwenye ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa zamani wa tawi hilo, Angel Akilimali akiendesha kikao cha uchaguzi
Angela akimpongeza Mwenyekiti mpya Mary Nchimbo baada ya matokeo

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª