.

VIONGOZI YANGA WAZIDI KUIKIMBIA SIMBA

Apr 24, 2012


Wakati Yanga ikisubiriwa kwa hamu kuingia katika mdomo wa Simba katika mechi ya lala salama ya Ligi Kuu ya Vodacom, timu hiyo imezidi kugubikwa na changamoto kibao.
     Taarifa zilizoripotiwa na Mapipiro Blog, zimesema viongozi wengine wawili muhimili ndani ya klabu hiyo yenye makao yake makuu mtaa wa Jangwani, jijini Dar es Salaam, wametangaza kujiuzulu.
     Kwa mujibu wa Blogu hiyo, viongozi hao ni pamoja na mumbe wa kamati ya utendaji ya Yanga Seif Ahmed na mjumbe wa Kamati ya Ufundi, mashindano na usajili, Abdallah Binkleb.
  "Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Yanga zinaeleza kuwa viongozi hao wameamua kubwaga manyanga baada ya kuchposhwa na ubabaishaji unaofanywa na baadhi ya viongozi wa juu wa klabu hiyo na tayari wameshawasilisha barua kwa Mwenyekiti wa yanga, Lloyd Nchunga".

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช