Na Pardon Mbwate na Felister, wa Jeshi la Polisi -Kigoma
JESHI la Polisi mkoani Kigoma leo
limewafukuza kazi askari wake wanne kwa tuhuma za kudai na kupokea
rushwa ya dola 300 za Kimarekani kutoka kwa raia mmoja wa China kinyume na maadili ya Jeshi hilo.
Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma Frasser Kashai amewataka mwenye namba E.3890 CPL Admirabils Malaso(43), G. 814 PC Waziri Juma Rashidi(30) G. 3012 PC Makasi Edwin(25) na G. 3322 PC Elias Zakaria(24) ambao wote walikuwa wakifanyia kazi katika kituo cha Polisi Uvinza wilaya ya Kigoma Vijijini.
Kamanda
Kashai amesema kuwa mnamo Aprili 1, 2012 majira ya saa 5.00 usiku
askari hao wakiwa zamu katika kituo hicho cha Polisi Uvinza, walipokea
taarifa kwa njia ya simu ya mkononi kutoka kwa dada mmoja aitwaye Mary
Kapele(26) akiwaeleza kuwa yuko katika nyumba moja ya kulala wageni ya Manchester na alikuwa na Raia mmoja wa
Kichina mmoja wa wasimamizi wa ujenzi wa barabara ya kutoka Kigoma
Uvinza na kwamba waende kumshika ugoni ili wajipatie fedha na baadaye
kugawana na dada huyo.
Askari hao walikwenda katika nyumba hiyo ya kulala wageni na kumkamata Mchina huyo aitwaye Mafutao War, akiwa pamoja na dada huyo kisha wakamtaka atoe fedha kama
malipo ya kumshika ugoni na ndipo walipopewa kiasi cha dola 300 za
kimarekani na shilingi 10,000 za Kitanzania na kumuachia. Kamanda kashai
amesema kuwa mlalamikaji Bw. War alikuwa ni mkandarasi wa ujenzi wa
barabara ya Kigoma Uvinza.
Kamanda
Kashai alisema baada ya kuona tukio hilo, raia wema walitoa taarifa
Polisi mkoani Kigoma ambapo askari hao walikamatwa na baada ya uchunguzi
kufanyika walibainika kuwa walihusika na tukio hilo na ndipo
waliposhitakiwa kijeshi na kupatikana na hatia ya kufanya Kitendo kibaya
kinyume na mwenendo mwema wa Jeshi la Polisi.
Amesema
kufuatia hukumu hiyo ameamua kuwafukuza kazi kwa fedheha ili iwe
fundishi kwa askari wengine kufuata utaratibu na sheria katika utendaji
wa kazi zao za kila siku.
Kamanda Kashai amesema Koplo Admirabils Malalo ambaye alizaliwa Julai 1, 1969 katika kijiji cha Kilando wialaya ya Nkasi mkoani Rukwa, alijiunga na Jeshi la Polisi Julai 26, 1991 na hadi anafukuzwa amelitumikia Jeshi hilo kwa muda wa miaka 11, Kostebo Waziri Juma Rashidi alizaliwa Julai 1, 1982 katika kijiji cha Maisaka wilaya ya Babati mkoani Manyara, na alijiunga na Jeshi la Polisi Februari 05, 2007 na hadi kufukuzwa kwake alikuwa amelitumikia Jeshi la Polisi kwa muda wa miaka mitano.
Amesema
Konstebo Makasi Edwin ambaye alizaliwa Februari 28, 1987 huko kwenye
eneo eneo la Mabatini mjini Mwanza la na kujiunga na Jeshi la Polisi
Juni 28, 2009 amelitumikia Jeshi hilo kwa muda wa miaka mitatu na
Konstebo Elias Zakaria ambaye alizaliwa mwaka Julai 1,
1988 huko katika eneo la Nguvumali mjini Tanga na alijiunga na Jeshi la
Polisi Juni 28, 2009 ambaye naye pia amelitumia Jeshi hilo kwa muda wa
miaka mitatu tu.
Kamanda
kashai amesema kuwa Jeshi la Polisi halitasita kumchukulia hatua kali
za kisheria na hata kumfukuza kazi askari yeyote atakayebainika kwenda
kinyume na maadili ya Jeshi hilo iki ni pamoja na kujihusisha na vitendo
vya utovu wa nidhamu, uhalifu ukiwemo wa kudai na kupokea rushwa.
Taarifa hii ni kwamujibu wa Afisa Habari Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Inspekta Mohammed Mhina.
0715 886488, 0784 886488
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269