.

MWAKITABU AAGWA, AZIKWA LEO DODOMA

Apr 12, 2012

 Vijana wa CCM wakibeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Ofisa Mwandamizi wa Makao Makuu ya CCM, Gordon Mwakitabu kuliingiza nyumbani kwa marehemu, eneo la Area C, mjini Dodoma leo, kwa ajili ya kuaga na mazishi yaliyofanyika baadaye kwenye makaburi ya Nkhungu nje kidogo ya mji. Aliyebeba msalaba ni mtoto wa kwanza wa marehemu Mwakitabu, Martin Mwakitabu.
 Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama (katikati) akizungumza na Makatibu Wakuu wastaafu wa CCM, Philip Mangula (kushoto) na Yussuf Makamba, wakati wa shughuli za maziko ya aliyekuwa Ofisa Mwandamizi Makao Makuu ya CCM, Gordon Mwakitabu mjini Dodoma leo.
 Mjane wa Gordon Mwakitabu, Janeth Mwakitabu akiangua kilio wakati wa kuaga mwili wa marehemu mumewe, leo nyumbani kwao, Area C, mjini Dodoma.
 Waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu Mwakitabu wakati wa kuaga.
 Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama akiaga mwili wa marehemu mwakitabu.
 Makatibu wakuu wastaafu wa CCM, Yussuf Makamba na Philip Mangula wakiuaga mwili wa marehemu Mwakitabu.
 HUZUNI! Waombolezaji wakiwa katika huzuni na mshangao, wakati wa kuaga mwili wa marehemu Mwakitabu. Waliokaa mbele, Kutoka Kushoto ni Katibu wa NEC, Mambo ya Nje, Januari Makamba, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), John Chiligati.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa na Maofisa Waandamizi wa makao makuu ya CCM kwenye msiba huo
 Mjane wa marehemu Mwakitabu akifarijiwa wakati yupo na watoto wa marehemu wakati wa kuaga
 Nape na Aggrey Mwanri wakiuaga mwili wa marehemu Mwakitabu
Watoto wa marehemu wakiuaga mwili wa marehemu baba yao

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª