Breaking News

Your Ad Spot

Apr 20, 2012

NIMR YAFANIKIWA KUGUNDUA KIFAA KIPYA


NA ROSE JAKSON,ARUSHA
TAASISI  ya taifa ya  utafiti ya magonjwa ya binadamu (NIMR) imegundua  kifaa kipya kijulikanacho kama Genexpert kwa ajili kupima  ugonjwa wa kifua kikuu(TB)

Akizungumza katika mkutano wa 26 wa taasisi ya tafiti wa magonjwa ya binadamu(NIMR)mratibu wa tafiti za kifua kikuu katika kituo cha NIMR Mbeya  Dkt.Elias Nyanda alisema kuwa kifaa hicho kimethibitishwa  na shirika la afya ulimwenguni(WHO).

 Alisema kuwa kifaa hicho cha kisasa kina gundua vimelea vya kifua kikuu vyenye vina saba ambavyo vinagundua wadudu walioko kwenye ugonjwa wa kifua kikuu ndani ya masaa mawili na mgonjwa akapata majibu yake.

Aidha alisema kuwa faida ya kifaa hiki cha kisasa ni pamoja na kugundua  kifua kikuu na usugu wa dawa  ambapo kifaa kilichokuwa kinatumika awali cha darubini hakikuwa na uwezo huo.

Faida nyingine ni kupunguza uwezo wa kuambukiza ugonjwa huo ambapo hapo awali wagonjwa wa kifua kikuu  walioonekana kuwa na ugonjwa huo lakini baada ya kupimwa wakaonekana hawana kwa asilimia 60.

“Kifaa hiki kinagundua kwa haraka sana usugu mwingi ambao mgonjwa amekaa nao kwani mtu akiachwa bila kutibiwa ni wazi kuwa atasambaza mapema kwa watu wengine”alisema Nyanda.

Hata hivyo alitaja changamoto zinazowakabili kutokana na kifaa hicho kuwa ni pamoja na gharama kubwa sana lakini watengenezaji na mashirika ya kifedha wanajaribu kupunguza bei kwa nchi zinazoendelea ili kila nchi iweze kuwa na kifaa hicho.

Mbali na hayo alisema kuwa mkoa wa Dar es salaam ni miongoni mwa mkoa unaoongoza kuwa na wagonjwa wengi wa kifua kikuu kwa kuwa tafiti zinaonyesha kuwa asilimia nyingi wa wagonjwa ndiko wanapotokea.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages