.

SERENGETI YAZINDUA PROMOSHENI YA 'VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO'

Apr 22, 2012

KAMPUNI ya Bia ya Serengeti (SBL) imewahimiza Watanzania kushiriki kwa nguvu  zote katika promosheni ya 'Vumbua Hazina ya Chini ya kizibo' ili kuweza kushinda zawadi kibao ziizotengwa.
Akitoa mwito huo  Mkurugenzi wa Masoko wa Kambpuni ya SBL, Ephrahim Mafuru amesema SBL imetenga kitita cha jumla ya sh. Milioni 783 kwa ajili ya kuwazawadia washindi mbalimbali wa promosheni hiyo  itafanyika kwa wiki 16 kuanzia Aprili 22 mwaka huu.
Mafuru alisema kuwa zawadi kwa wale watakao jishindia zawadi ya bia zina thamani y ash. Milioni 265 zawadi za fedha taslim ni sh. Milioni 383. Alisema kuwa pia watatoa pikipiki 16, Bajaj inane (8) , Jenereta nane (8) na magari matatu aina ya Ford Figo.
 Alisema kuwa ili kuweza kuingia katika shindano hilo unatakiwa kununua bia zao, Serengeti, Tusker au Pilsner  na kukuta neno  lenye tarakimu saba na kulituma kwenda namba maalum ya 15317 na kuingia katika shindano hilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Push Mobile, Freddie Manento aliipongeza SBL kwa kuiteua kampuni yake kuendesha shindano hilo hasa kwa kuzingatia ubora wa huduma zake.
Manento alisema kuwa kampuni yao ni bora zaidi katika kuendesha zoezi kama hilo na kuahidi kutoa hudima bora kwa wateja wake.
“Ni faraja kubwa kufanya kazi na SBL katika shindano hili kubwa la kuwazawadia wateja wa bidhaa zinazozalishwa na kampuni hiyo ya bia, tutafikisha lengo lililowekwa,” alisema Manento.


 Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Ephraim Mafuru kionyesha zawadi zinazoshindaniwa kwenye promosheni ya 'Vumbua Hazina chini ya kizibo', wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo le, kwenye hoteli ya Serena, Dar es Salaam. Wengine kushoto ni Mkurugenzi wa Biashara SBL, Asia Mhina na wapili kulia ni Meneja Bia ya Serengeti  Maurice Njowoka
Wadau wakiwa kwenye uzinduzi wa promosheni hiyo.0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª