Breaking News

Your Ad Spot

Apr 19, 2012

SERIKALI KUWEKEZA KATIKA TAFITI ZA MAGONJWA

Na Rose Jackson, Arusha
SEREKALI imesema kuwa kwa sasa inawekeza zaidi katika masuala ya tafiti  za magonjwa mbalimbali jambo ambalo litaweza kupunguza na kuhudumia vema jamii mbalimbali za watanzania 

Hayo yamebainishwa jijini hapa na Makamu wa Raisi wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Gharib Bilal wakati akifngua mkutano kongamano la 26 kwa wadau wa taasisi  ya utafiti wa magonjwa ya binadamu(NIMR) mapema jana

Dkt Bilali alisema kuwa kwa mfumo huo wa Serikali kuweza kuwekeza zaidi katika tafiti za magonjwa ya binadamu kutasaidia kwa kiwango kikubwa sana hata kupata vyanoz halisivya magojwa ambayo yanasumbua Jamii

Aliongeza kuwa mbali na kufanikiwa kuwekeza zaidi katika masuala ya tafiti ambayo yanafnywa na baadhi ya watafiti hapa nchii lakini pia Serikali nayo imejipanga kuhakikisha kuwa inaendelea kuwa na wataalamu wengi zaidi ambao nao kwa kiwago kikubwa sana wataweza kusadia jamii

“kwa sasa tumejipanga kuhakikisha kuwa kila mahala tunakuwa na watafiti ambao wataweza kufanya chunguzi mbalimbali na kasha kubaini vyanzo hali ambayo itatufanya tuweze kufikia malengo yetu ya kupambana na aina mbalimbali za magonjwa ambayo tumekusudia

Pia aliongeza kuwa kwa sasa Serikali nayo imefanikiwa kukabiliana na changamoto mbalimbali ambazo zimo kwenye jamii kama vile vifo vya mama na mtoto, pamoja na gonjwa ambalo lilikuwa linasumbua sana ,Malaria

Alifafanua kuwa kwa sasa ndani ya changamoto hiyo magonjwa ya Malaria yamepungua kwa kiwango cha hali ya juu sana pamoja na vifo vya mama na mtoto jambo ambalo ni faraja kwa Serikali kutokana na malengo yake ambayo yamekusudiwa

Awali mkurugenzi mkuu wa taasisi hiyo ya  taifa ya utafiti wa magonjw yabinadamu , Dkt Mwele Malecela  alisema kuwa kwa sasa ndani ya nchi ya Tanzania kuna umuhimu mkubwa sana wa watalaamu kuweza kufanya tafiti  ambazo zitakuwa pamoja na Takwimu hali ambayo itachangia kwa kiwango kikubwa sana  watalamuj hao kuweza kufanya kazi kwa uraisi sana.

Dkt Mwele alisema kupitia Tafiti na Takwimu za magonjwa mbalimbali wataweza kujua na kubaini kasi ya magonjwa hata yanayoambukiza kwa kasi sana jambo ambalo nalo litaweza kupatiwa ufafanuzi kwa ikwiango cha juu sana.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages