Breaking News

Your Ad Spot

Apr 28, 2012

WAKUU WA EAC WAKUTANA ARUSHA LEO


NA MWANDISHI WETU, ARUSHA
Wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wanatarajiwa kukutana  Arusha, hii leo, katika mkutano maalum utakaojadili pamoja na mambo mengine, mapendekezo ya maombi ya nchi ya Sudan Kusini, kujiunga na jumuiya hiyo.
Nchi zote tano za Kenya, Uganda, Tanzania,Rwanda na Burundi zinatarajiwa kuhudhuria mkutano huo wa siku moja utakaofanyika katika hoteli ya Ngurdoto, nje kidogo ya mji wa Arusha.
Taarifa zilizopatikana toka ofisi ya EAC,Idara ya Mawasiliano na Masuala ya Umma imesema mkutano huo pia unatarajiwa kujadili agenda nyingine nne.
Maombi ya Sudani Kusini yatafikiriwa ikiwa ni miezi karibu mitano baada ya maombi ya Jamhuri ya Sudani kukataliwa kwa madai ya kutokidhi vigezo vilivyoanzisha mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mkataba huo unaeleza wazi kwamba nchi yoyote inayotaka kujiunga na EAC, sharti iwe imepakana na moja kati ya nchi tano wanachama wa jumuiya hiyo.
Hata hivyo maombi ya Sudani Kusini yanakuja wakati ambapo ipo katika hali ya uwezekano wa kuingia katika vita kamili na jirani yake, Sudani Kaskazini, hoja ambayo huenda pia itatupiwa jicho na kikao hicho cha Wakuu wa EAC.
Nchi hiyo mpya kabisa barani Afrika na duniani kwa ujumla, ilipatikana Julai 1, 2011 baada ya mwongo mmoja wa vita na Sudani Kaskazini.
Hoja nyingine ambazo zinatarajiwa pia kujadilia katika mkutano huo ni pamoja na uteuzi wa Naibu Katibu Mkuu mpya wa EAC, atakayeshughulikia Shirikisho la Kisiasa, kuchukua nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Beatrice Kiraso wa Uganda ambaye kamaliza mkataba wake wa kazi na pia kufikiria kumwongezea mkataba wa kazi, Naibu Katibu Mkuu, anayeshughulikia Uzalishaji na Sekta ya Jamii, Jean Claude Nsengiyumva kutoka Burundi.
Mkutano huo wa Wakuu wa EAC, umetanguliwa na mkutano maalum wa 24 wa Baraza la Mawaziri wa EAC.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages