Mafisango |
Aliyekuwa mchezaji wa Simba, Patrick Mafisango amefariki dunia kwa ajali ya gari mjini Dar es Salaam.
baada ya kupata ajali usiku wa kuiamkia leo katikan eneo la Tazara.
Taarifa zinasema katika ajali hiyo Mafisango alikuwa na familia yake akitoka Klab, na kwamba familia yake ambao idadi yao haikutajwa wamepata majeraha.
Mafisango alikuja kucheza soka nchini Tanzania akitokea Rwanda na alikuwa mchezaji wa timu ya taifa ya nchi hiyo Amavubi.
Kwa mara ya kwanza alisajiliwa na timu ya Azam kwa mkopo na baadaye kusajiliwa na Simba baada ya kubadilishwa na mchezaji Hamid Humud.
Baada ya kumaliza mkataba wake Mafisango alisajiliwa tena Simba na hadi anafariki dunia alikuwa mchezaji wa kutumainiwa wa kikosi hicho ambacho sasa ni mabingwa wa Soka Tanzania Bara.
Mafisango ambaye ni raia wa Rwanda alizaliwa mjini Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (Congo-DRC) Machi 9, 1980
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269