.

MWILI WA MAFISANGO KUAGWA KESHO TCC CLUB, CHANG'OMBEA

May 17, 2012

Aliyekuwa kiungo maili wa Simba na timu ya Taifa ya Rwanda (Amavubi),  Patrick Mutesa Mafisango (pichani) aliyefariki kwa ajali ya gari alfajili ya leo katika eneo la Veta Keko jijini Dar es Salaam, anatarajiwa kuagwa kesho.

Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Simba Godfrey Nyange Kabulu amesema kuwa mwili wa marehemu Mafisango utaagwa katika viwanja vya Sigara (TTC CLUB), Chang'ombe jijini Dar es Salaam kuanzia majira ya saa 2:00 asubuhi na kusafilishwa Mei 19 kwenda kwao Congo DRC kwa mazishi.

Habari katoka katika eneo la tukio zimesema kuwa ajali hiyo imetokea baada ya kumkwepa mwendesha pikipiki na kisha gari la Mafisango kupinduka.
Watu wengine watano waliokuwa na Mafisango walijeruhiwa vibaya wakati wakitoka katika Ukumbi wa Maisha Klabu Masaki jijini Dar es Salaam akiwa na marafiki zake wavulana watatu na wasichana wawili .
“Msiba huu ni pengo kubwa kwa Simba kutokana na umuhimu wake akiwa uwanjani hivyo basi sina mengi ya kusema zaidi ya kuwa na pigo mara baada ya kuondokewa na mchezaji mahili katika timu yetu”alisema Kabulu.
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha mchezaji huyo na kusema kuwa ni Msiba mkubwa kwa familia ya Soka kwani Mafisango kwa kipindi chote alichocheza mpira hapa nchini akiwa na timu ya Azam na baadaye Simba, aliifanya kazi yake ya kucheza mpira kwa bidii.
Ofisa habari wa TFF Boniface Wambura alisema kuwa kifo cha nyota huyo ni pigo kubwa si tu kwa familia yake na timu alizochezea, bali ukanda mzima wa Afrika Mashariki na Kati ambapo changamoto zake zilikuwa dhahiri uwanjani.
Wambura alisema wakati mauti yanamkuta, Mafisango alikuwa ameitwa Amavubi kwa ajili ya mechi za mchujo za Kombe la Dunia, Kanda ya Afrika zinazochezwa mapema mwezi ujao.

“TFF inatoa pole kwa familia ya Mafisango, klabu ya Simba, Shirikisho la Mpira wa Miguu Rwanda (FERWAFA) na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito”alisema Wambura na

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª