Breaking News

Your Ad Spot

Jun 13, 2012

MISS DAR INTER COLLEGE KUTEMBELEA MAKUMBUSHO YA TAIFA J'MOS

Na Mwandishi Wetu 
Warembo wanaotarajiwa kushiriki shindano la Miss Dar Intercollege 2012  jumamosi  hii wanatarajiwa kutembelea makumbusho ya Taifa kwa ajili ya kujifunza. 
     Shindano hilo linatarajiwa kufanyika katika ukumbi huo wa Makumbusho ya Taifa uliopo mkatabala na chuo cha usimamizi wa Fedha (IFM) Juni, 22 mwaka huu.
     Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, mratibu wa shindano hilo Dina Ismail, alisema ziara hiyo itawasaidia sana warembo hao katika harakati zao za kielimu.
    Alisema Makumbusho ya Taifa ni sehemu muhimu kwa kila Mtanzania kufahamu kutokana na kuwepo vitu vingi vya kihistoria vilivyopata kutokea katika karne zilizopita.
    Kama mjuavyo kule kuna kuna fuvu la mtu wa kwanza duniani (zinjathropas), vyombo, magari na vitu vingine vya kwanza kuanza kutumika,”alisema.
     Dina aliongeza kuwa maandalizi kwa ajili ya shindano hilo yanakwenda vema ambapo washiriki 13 kutoka vyuo vya IFM, Ustawi wa Jamii, Chuo Cha Biashara (CBE), uandishi wa Habari (DSJ) na Huria (OUT) wanaendelea na mazoezi kwenye hoteli ya The Grand Villa iliyopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam. 
    Warembo hao ambao wapo chini ya ukufunzi Marlydia Boniface na Bob Rich ni  pamoja na Veronica Ngota, Rose Muchunguzi, Nancy Maganga, Hilda  Edward, Diana Nyakisinda, Neema Michael, Veronica Yollla, Jacquiline Cliff, Sharifa Ibrahim, Natasha Deo, Saada Suleiman, Rose Masanja na Jamila Hassan. 
    Shindano hilo limedhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia kinywaji cha Redd’s Original, Dodoma Wine, Ndege Insurance, Shear Illusions, Skylight Band, Lamada Hotel, Screen Masters, Makumbusho ya Taifa, Mustafa Hassanali, Grand Villa Hotel, Clouds Fm na blog za Michuzi, Mamapipiro, Bin Zubeiry, Mtaa kwa Mtaa na Full Shangwe.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages