.

PALESTINA INAPOAMUA KUWA NGANGARI UMOJA WA MATAIFA

Jul 4, 2012

 Sasa wakisema tunapiga kura   hapa pame kaa vipi, ndivyo anavyoonekana kusema,  Brigedia General Charles Muzanizanila kutoka  Jeshi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ ) akiwa katika  majadiliano na Kaimu Balozi wa  Ubalozi wa  Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Justin Seruhere. Dkt. Seruhere na Brigedia  General Muzanizanila wanaongoza  ujumbe wa Tanzania katika  mkutano wa mwezi mmoja wa   nchi Wajumbe wa majadiliano kuhusu Mkataba wa  Biashara ya Silaha ( ATT). viongozi hawa wawili   kama ilivyokuwa kwa wajumbe wengine, walijikuta wakitafakari hatima ya maendeleo ya mkutano huu, baada ya kutokea mkwamo uliosababishwa na nchi ya Misri kuamua kuwasilisha hoja siku ya kwanza  ya kuanza kwa mktano huo ( jumatatu) hoja ya kutaka  Ujumbe wa Palestina uruhusiwe kushirika mkutano huo kama nchi kamili na si mtizamaji (observa)
 Wajumbe wa mkutano wa  majadiliano kuhusu mkataba wa biashara ya silaha ( ATT) wakiwa katika mkanganyiko wa kutoa jua nini hasa kilikuwa kikiendelea baada ya kuahirishwa kuanza kwa majadiliano kutona na mvutano mkali wa kidiplomasia uliosababishwa na  hoja iliyowasilishwa na Misri kutaka Palestina ishiriki kama nchi kamili.  Palestina ilishikilia msimamo huo kiasi cha kuufanya mkutano huo kushindwa kuanza kwa wakati. lakini hatimaye suluhu ilipatikana  na  Palestina ikaruhusiwa kushiriki kwa asili mia kwa mia. HABARI KWA KINA BONYEZA HAPA

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª