.

WAZIRI KABAKA ALONGA UMOJA WA MATAIFA

Jul 4, 2012

 Gaudentia Mugosi Kabaka ( MP)  Waziri wa Kazi na Ajira  akizungumza wakati wa mkutano wa  Umoja wa Mataifa unaojadilini pamoja na mambo mengine tatizo la ajira na hasa kwa vijana, Mhe. Kabaka anaongoza ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mkutano huu wa wiki moja, ukiwashirikisha  mawaziri wanaohusika na masuala ya ajira, fedha na uchumi, mambo ya nje ,   ILO na wanazuoni.  katika mchango wake kuhusu changamoto hiyo ya  ukosefu wa ajira, Mhe. Waziri Gaudentia Kabaka anasema kama ilivyo kwa nchi nyingine zinazoendelea. Tanzania pia inakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa ajira na kwamba serikali imekuwa ikichukua hatua mbalimbali za kujaribu kulikabili tatizo hilo ambalo limekuwa ni changamoto kubwa kwa mataifa tajiri na  maskini pia na ni bomu ambalo limeshaanza kufuka moshi.

Baadhi ya ujumbe wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano huu unaojadili tatizo la ajira, ni  mkutano ambao umeandaliwa na Baraza la Umoja wa Mataifa  linalohusika na masuala ya Uchumi na Maendeleo ya Jamii maarufu kama   ECOSOC.  Walio kaa mbele ni  Kamishna. Ahmed Makame Haji,  kutoka Tume ya  Mipango  Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bw. Omar Hamisi Same kutoka Wizara ya Kazi na Ajira,  Bi. Aziza J. Ali, Mkuu wa kitengo kinachoratibu misaada,  Idara ya Fedha za Nje, Serikali ya  Mapinduzi Zanziba na  Bw. Humphrey Shangarai, mchumi kutoka Idara ya Sera na Mipango, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa  Kimataifa. Habari Kamili BOFYA HAPA

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª