Breaking News

Your Ad Spot

Sep 11, 2012

SIMBA YAILAMBA AZAM 3-2 NGAO YA JAMII

 Mlinda mlango wa timu ya Simba, Juma Kaseja, akionyesha Ngao ya Jamii, ambayo timu hiyo imekabidhiwa na Naibu Waziri wa  Kazi na Ajira, Makongoro Mahanga jioni hii, baada ya timu hiyo kuinyuka Azam FC mabao 3-2 katika mchezo wa kuwania ngao hiyo, uliopigwa  kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Simba imeibuka na ushindi baada ya kuwa imeteswa na Azam katika kipindi cha kwanza, kwa sababu kipindi hicho kilimalizika ikiwa imebebeshwa mabao 2-1.
  Lakini Katika kipindi cha pili, Simba walifanya mabadiliko makubwa ya kiuchezaji kiasi kwamba kibao kiliwageukia Azam, ambapo Simba walirudisha bao la kusawazisha na kisha kuwapiku Azam kwa kujipatia bao la ushindi la tatu katika kipindi hicho cha pili.
Picha zaidi;- BOFYA HAPA UKURASA WA SPOTI

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages