Breaking News

Your Ad Spot

Sep 11, 2012

MAANDAMANO YA WAANDISHI DAR KULAANI MAUAJI YA MWANGOSI

 Mwandishi Lauden Mwambona akiwa amegunga mdomo kama hivi wakati wa maandamano hayo
 Waandishi wakiwa nje ya ofisi za Channel Ten jijini Dar es Salaam, kabla ya maandamano hayo
 Hawa nao wakati mmoja ameziba mdomo, mwenzake akaziba macho kufikisha ujumbe wa kulaani mauaji ya Mwangosi
 Hamis Kibari na Hamis Mzee, wakijadiliana jambo kabla ya maandamano kuanza kwenye ofisi za Channel Ten
 Hili ni moja ya mabango waliyokuwa nayo waandishi
 Jese Kwayi, Mzee Maro na mwezake wakiwa kwenye maandamano hayo
 Mpigapicha huyu akifanya jitihada za kupata picha nzuri za waaandamanaji
 Maandamano yakitoka Ofisi za Channel Ten kupitia Morogoro Rd
 Ujumbe mwingine ni huu unaoelekezwa kwa Afande Mwema
 Polisi akiwacheki kwa baaali wakati maandamano ya waandishi  yakikatiza Barabara ya Bibi Titi Mohammed
 Huyu ni Manyerere Jackton na bango lake
 Polisi wakiwasindikiza waandamanaji, eneo la Fire
 Waandishi wakiingia viwanja vya Jangwani
 Kada wa Chadema (siyo mmoja wa waandishi wa habari) Dk. Azaveri Lwaitama ambaye ameshiriki maandamano hayo, akijadiliana jambo na Nyaronyo Kicheere kuhusu mambo mbalimbali wakati, baada ya maandamano kufika Viwanja vya Jangwani.
" Dk. Nchimbi ondokaaaaa" mwandishi akipaza sauti kuungana na wenzake waliokuwa wanamkataa kuwepo Dk. Nchini.
 Dk. Nchini akajaribu kuwatuliza... waandishi bila mafanikio.
 Kisha Dk.Nchimbo akaondoka akisindikizwa na viongozi wa Jujwaa la Wahariri
 Baada ya waziri kuondoka, viongozi wa waandishi wakaanza kuzungumza. Huyu ni Jame Mihanji wa Kbabu ya Waandishi ya Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Muungano wa vyombo vya habari Karsan akizungumza kwenye mkutano huo
 Viongozi wahahanikiza kulaani mauaji ya Mwangosi
 Nevil Meena wa Jukwaa la Wahariri akizungumza
 Waandishi waliokwenda katika maandamano hayo inaonyesha walikuwa kikazi kweli kweli.... Cheki hili buti...
 Waandishi wa Uhuru FM wakifuatilia
 Jane Mihanji akiimbisha wimbo la Solidality Forever
Kada wa Chadema, Dk. Lwaitama ambaye ameelezwa kuwa rafiki wa wanahabari akizungumza baada ya kukaribishwa jukwaani. Habari Kamili:BOFYA HAPA SASA

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages