Breaking News

Your Ad Spot

Oct 28, 2012

CHADEMA YABAKI YATIMA NJOMBE, IRIMBA NA MBEYA


*MLEZI KATIKA MIKOA HIYO AJIVUA UANACHAMA KUEPUKANA NA KINA  MBOWE NA DK. SLAA
MBEYA, TANZANIA
CHADEMA kimebaki yatima katika mikoa ya Njombe, Mbeya na Iringa kufuatia aliyekuwa mlezi wa chama hicho katika mikoa hiyo, Thomas Nyimbo, kujivua  rasmi uanachama.

Nyimbo ambaye alikuwa nguzo muhimu kwa uhai wa Chadema katika mikoa hiyo, katika kujivua uanachama amesema  ni kwa sababu ya kuchoshwa na ubabaishaji uliopo miongoni mwa viongozi wakuu wa chama hicho huku akiwavurumishia lawama, Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dk.Willbroad Slaa kwamba wamekuwa wakitumia chadema kama SACCOS yao ya kujipantia manufaa binafsi.

Akizungumza leo katika ukumbi wa hoteli ya Mount Livingstone mjini Mbeya, Nyimbo alisema ameamua kujivua uanachama baada ya kuona CHADEMA kinakwenda kinyume na malengo yake kama kinavyojipambua mbele ya umma wa watanzania.

Alitumia nafasi hiyo kuwataka vijana nchini kupigania maslahi yao kwa mtazamo chanya wenye kuleta mustakabari mzuri kwa Taifa, badala ya kufikiri kuwa mabadiliko ni kuiondoa CCM madarakani na kuiweka CHADEMA

“Licha ya CHADEMA kujaribu kuwaaminisha watanzania hasa vijana kuwa ndio chama chenye kuleta mabadiliko ya kweli, lakini Mwenyekiti Mbowe na Katibu Mkuu Dk.Slaa wamekuwa wakikitumia kujinufaisha wao binafsi” alisema Nyimbo.

Aliongeza  viongozi hao wakuu pia wamekuwa siyo watu wa kushaurika ndani ya chama huku kikbaya zaidi wakiendesha siasa katika mfumo mbaya wa kushawishi na kuaminisha jamii bila ya kuwa na suluhisho.

Nyimbo aliongeza siasa za namna hiyo ni hatari kwa Taifa, kwani baada ya kuungwa mkono kwa kiwango cha juu na kundi la vijana kwa imani ya kukombolewa pale watakapofanikiwa kushika dola, na kushindwa kutimiza vurugu kubwa zitalipuka nchini.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages