Amina Makillagi |
DODOMA, TANZANIA
KITIMU timu cha Uchaguzi Mkuu wa Jumuia ya Wanawake Tanzania(UWT) kinaanza lesho Mkutano Mkuu wa Jumuia hiyo utakapoanza.
Wakati joto likiwa limeshapanda miongoni mwa wanaowania nafasi mbalimbali za uongozi katika Jumuia hiyo, UWT imeapa kumpoka mshindi mgombea yeyote atakayebainika kujihusisha na rushwa au kampeni za kupakana matope.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma, Makillagi amesema ingawa mpaka sasa hakuna taarifa rasmi za kuwepo kwa vitendo vya rushwa miongoni mwa wagombea lakini, atayekegundulika atapokonywa ushindi bila kujali ameshinda kwa kura kiasi gani.
"Kama ilivyokawaida yetu na kanuni na maadili yetu yanavyosema kuwa yeyote atakayebainika kujihusisha na rushwa au kampeni za kupakana matope hatutasita kumpoka uongozi alioupata'' alisema.
Alisema ni vyema wagombea wote wakafuata kanuni katika uchaguzi huo kwa kujiepusha kwa vitendo vya rushwa wasipokee wala kutoa rushwa kwa wagombea.
Akizungumzia matayarisho ya mkutano huo Katibu Makilagi alisema mkutano huo unatarajiwa kufunguliwa na Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal na kufungwa kesho na Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Kikwete.
Alisema baada ya ufunguzi huo Mkutano huo utapokea salaamu toka vyama marafiki kikiwemo ANC,Zanu PF, Angola, Namimbia Rwanda,Burundi na Kenya.
Katika viwanja vya Makao Makuu ya CCM Dodoma wapambe wa wagombea walionekana wakigawa vipeperushi huku kila mmoja akimnadi mgombea wake.
Katika Mkutano huo nafasi mbalimbali zitagombewa ikiwemo nafasi ya mwenyekiti wa UWT ambayo inagombewa na wagombea watatu ambao ni Sophia Simba, Mayrose Majige na Ane Kilango Malecela, huku nafasi ya Makamu wakichuana Asha Abdallah Juma na Asha Bakar Makame.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269