Breaking News

Your Ad Spot

Nov 12, 2012

HAPA NA PALE KATIKA PICHA KIZOTA

 Mkutano Mkuu wa Nane wa CCM, pia umetoa fursa kwa baadhi ya wajasiriamali kuutumia kufanya biashara. Hili ni moja ya mabanda kwenye Viwanja vya Ukumbi wa Kizota mjini Dodoma
 Mtangazaji wa Uhuru FM, Steve Mhina akimhoji Mhariri wa gazeti la Mzalendo, Bakari Mnkondo kuhusu yanayojiri kwenye banda la Kampuni ya Uhuru Publications Ltd, Wachapishaji wa magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Burudani, ambalo limo kwenye viwanja vya Kizota kuhajihisha mkutano huo
 Mobu la Vijana kutoka Makao Makuu ya Umoja wa Vijana wa CCM, jijini Dar es Salaam, wakiwa kwenye viwanja vya Kizota. Katibu Mkuu wa UVCM Martine Shigela alikuwa mmoja wa wagombea wa NEC, Viti Kumi Bara
 Watu wakifuatilia kwenye TV yaliyokuwa yakijiri ukumbini, wakiwa wameketi raha mustarehe nje ya ukumbi wa Kizota
 Mamaaa Asha Baraka akitembelea banda la Uhuru Publications Ltd
 'Wataalam' wa  kuchoma nyama wakiwa kazini kwenye viwanja hivyo
 Baada ya pilika pilika za kusaka kura kwa ajili ya wagombea wao, baadhi ya wapambe wakijiliwaza kwa kiywaji kwenye mabanda yaliyopo katika viwanja vya Kizota
 Banda la maonyesho la Uhuru Publications linavyoonekana kwenye viwanja vya Kizot
 Makada wa CCM, wakiwa nje ya viwanja vya Kizota kufuatilia hali ya amambo Uwanjani. Kutoka kushotoKatibu wa CCM Nzega, Kajoro Vyohoroka, Mwenyekiti wa CCM Nzega, Amos Kameda, Mjumbe wa NEC Nzega Yassin Memba na Msaidizi Maalum wa Katibu Mkuu wa CCM, Edward Mpogolo.
"TUPIGE NA SISI PICHA TUONEKANE" ni Mjumbe wa Mkutnao Mkuu (UWT) kutoka Mara Agnes Mathew na Mjumbe wa NEC kutoka Katavi Kampala Maganga.

 Mhariri wa Mzalendo, Bakari Mnkondo akiwa na wafanyakazi wenzake wa Uhuru Publicatiosn Ltd Selina Wilson na  Latifa Ganzel kwenye banda la UPL kwenye Viwanja vya Kizota
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Vanessa Frank akipata maelezo ya dawa za maradhi mbalimbali za asili zinazouzwa na mjasiliamali Roda Forman kutoka Mbeya kwenye viwanja hivyo vya Kizota

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages