Breaking News

Your Ad Spot

Jan 17, 2013

MSIBA WA MAREHEMU JUDITH CHIKAKA WA CHUO KIKUU CHA ARDHI



Marehemu Judith Chikaka Mapunda enzi za uhai wake.
Mwili wa Judith Chikaka ukiwa umelazwa ndani ya Jeneza Pamoja na mwili wa marehemu Mtoto wake mchanga. Judith Chikaka amefariki siku ya Jumapili  ya tarehe 13/01/2012 katika Hospitali ya Mwananyamala wakati alipofikishwa hapo kwa ajili ya kujifungua, kwa bahati mbaya na mapenzi yake muumba akafariki kabla ya kujifungua.
Mume wa Marehemu Judith, Bwana Erasto Mapunda akiwa amembeba mtoto wake wa kwanza aliyezaa na mkewe. 
Baba mzazi wa marehemu Judith, Mzee Chikaka 
Mama mzazi wa marehemu Mama Chikaka sakiwana majonzi makubwa baada ya kumpoteza mtoto wake kipenzi 
Padre kutoka Parokia ya Kigamboni akiendesha Ibada ya misa takatifu ya kumwombea Judith alale kwa amani. Ibada hiyo ilifanyika nyumbani kwa Marehemu Judith maeneo ya Kigamboni Kibada. 
Baadhi ya viongozi wa CCM Temeke wakitoa salam zao za rambi rambi.
Spika wa Bunge la wanafunzi wa chuo cha Ardhi akitoa salamu za rambi rambi kwa niaba ya wanafunzi wenzake.
Rais wa Chama cha Riadha Tanzania Bwana S. Nyambui akitoa salamu za rambi rambi kwa niaba ya wanachama na chama chao kwa ujumla.
Mume wa marehemu Judith akiweka Shada la maua katika nyumba ya milele ya mkewe
Kushoto ni mwakilishi wa Familia ya marehemu akipokea rambi rambi kutoka kwa wafanyakazi wenzake wa marehemu kutoka wizara ya Ardhi
Mwakilishi kutoka Wizara ya Ardhi upande wa michezo akitoa salamu zake kwa niaba ya wanamichezo wenzake. 
 Hii ndio nyuma ya milele ya marehemu Judith Chikaka Mapunda ambamo amelazwa jana katika makaburi ya Kibada, Kigamboni, ameacha Mume na Mtoto mmoja.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages