Breaking News

Your Ad Spot

Feb 6, 2013

MAKANDARASI WADAIWA KUSHIRIKIANA NA VISHOKA KUHUDUMU HUDUMA ZA TANESCO MBEYA


MBEYA Tanzania
Shirika  la umeme Tanzania(Tanesco) Mkoa wa Mbeya limesema baadhi ya makandarasi wa shirika hilo kwa kushirikiana na vishoka wamekuwa wakiuza fomu za maombi ya umeme kinyume na utaratibu.

Meneja wa Tanesco Mkoa wa Mbeya Mhandisi .Julius Sabu amesema uchunguzi uliofanywa na uongozi wa shirika hilo,umebaini kuwa fomu moja huuzwa kati ya shilling 40,000-50,000 na watu wasiowaminifu badala ya sh 5900 ambayo ni bei harali ya shirika hilo.

Sabu alisema ili kukomesha hali hiyo uongozi wa Tanesco makao makuu  umeanzisha utaratibu kwa waombaji wote wa umeme wa awali kuja na picha wakati wa ujazaji fomu za maombi.

Hata hivyo,Kaimu Meneja huyo alisema fumu zote za maombi ya wateja hutolewa kutoka makao makuu na kuwa zimekuwa hazitoshelezi kulingana na mahitaji ya wateja kutokana na kumekuwepo  kwa  ongezeko kubwa la maombi ya wateja.

‘’unajua fomu tunazopata kutoka makao makuu hatizosherezi kulingana na mahitaji ya wateja na hii ni kutokana na kuwepo kwa ongezeko kubwa la maombi ya watu wanaohitaji umeme kwa mkoa wa mbeya.

Aidha alibainisha kuwa wastani wa maombi ya umeme kwa siku ni wateja 150 kwa wilaya ya Mbeya mjini tu na kuwa kwa mkoa mzima ni wastani wa maombi ya wateja zaidi ya 300 ikilinganishwa na hapo awali kabla ya kupitishwa kwa bei mpya za umeme, ambapo wastani wa wateja kwa siku ilikuwa ni 20 hadi  40 kwa wilaya ya mbeya mjini pekee.

Shirika la Tanesco Mkoa wa Mbeya limepewa malengo ya kuwaunganishia wateja 17,500 kwa mwaka ambapo Uongozi wa Tanesco wilaya ya Rungwe umewaunganishia wateja 167 kwa sasa kati ya malengo ya kuwaunganishia wateja 1750
kwa mwaka.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages