Breaking News

Your Ad Spot

Feb 18, 2013

ZIARA YA MAMA SALMA KIKWETE LINDI, LEO ALIKUWA KATA YA MBANJE

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mama Salma Kikwete, akiwahoji kwa nini walikuwa hawakwenda shule, wanafunzi wa shule ya msingi Kikwetu, wilaya ya Lindi mjini, walipokuwa kwenye mkutano wake wa hadhara uliofanyika, leo katika kijiji hicho. Kutoka kulia ni Said Martin (darasa la saba), Regina Fred na Rahma Mandunda wote wa darasa la sita. 
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mama Salma Kikwete, akimhoji kwa nini alikuwa hakwenda shule, mwanafunzi wa shule ya msingi Kikwetu, wilaya ya Lindi mjini, Asha Katiasi, aliyekuwa kwenye mkutano wake wa hadhara uliofanyika, leo katika kijiji hicho.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mama Salma Kikwete, akimkabidhi kadi ya CCM, mwanachama mpya Mwanaarafa Imani, alipopokea wanachama wapya 56 wakiwemo kutoka CUF, katiuka mkutano wake wa hadhara uliofanyika, leo katika kijiji cha Kikwetu, wilaya ya Lindi mjini. 
 Kina Mama wakinyoonyosha mikono kuikubali CCM, wakati wa mkutano ulifanywa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mama Salma Kikwete kwenye Kijiji cha Kikwetu, Lindi mjini mkoani Lindi leo. 
 Mama Salma Kikwete akikagua choo cha walimu kinachojengwa katika shule ya Msingi Kikwetu, wilaya ya Lindi mjini leo baada ya uongozi wa kata ya Mbanja ilimo shule hiyo, kuwambia kwamba kimejengwa kwa sh.. milioni 1.7
 Mama Salma Kikwete amekuwa kila mkutano wake kwenye ziara yake mkoani Lindi mjini anasikiliza maswali na maoni mbalimbali kutoka kwa wananchi na kisha kuyajibu au kutolea ufafanuzi na viongzi anaoambatana nao. Pichani, Mama Salma akisikiliza kwa makini alipokuwa akiulizwa swali na mwananchi mmoja, kwenye Mkutano wa Kijiji cha Kikwetu wilayani humo.
 Katibu wa CCM Kata ya Mbaje, Hamisi Limoja akiwatambulisha wajumbe kwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, wilaya ya Lindi mjini, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete alipowasili Kijiji cha Kikwetu katika kata hyo asubuhi hii, leo
Wajumbe wa Mkutano Mkuu Kata ya Mbaje, wakiwa kwenye mkutano wa ndani na Mama Salma Kikwete katika kijiji cha Kikwetu kata ta Mbaje.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages