.

MAKAMU MWENYEKITI WA CCM, MZEE MANGULA APATA MSIBA, AMEFIWA NA BINTI YAKE

Aug 18, 2013

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCCM), Taifa, Mzee Philip Japhet Mangula amepata msiba.

Habari tulizopata zinasema, Mzee Mangula amefiwa na Binti yake, Nemela Mangula (pichani), ambaye amefariki katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.


Pamoja na kufanya shughuli mbalimbali, Binti huyo amewahi kuwa Rais wa Wanafunzi alipokuwa akisoma Chuo Cha Diplomasia, Dar es Salaam.

Mzee Mangula
Hadi sasa waombolezaji wapo Masaki,  nyumbani kwa Mzee Mangula jijini Dar es Salaam, na bila shaka taarifa za kina kuhusu msiba huo zitapatikana. Timu nzima ya theNkoromo Blogu inachukua fursa hii kumpa pole za dhati Mzee Mangula kwa msiba huu.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช