Breaking News

Your Ad Spot

Nov 23, 2013

KINANA NA MSAFARA WAKE WAPANDA MV SONGEA KUTOKA MBAMBA BAY KWENDA KYELA

 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, asubuhi hii amemaliza ziara yake katika wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma na kuanza safari ya kwenda Kyela ambako ataanza ziara katika mkoa wa Mbeya. Pichani, Kinana na wajumbe wa sekretarieri ya CCM, Nape Nnauye (Itikadi na Uenezi) na Dk. Asha-Rose Migiro (Siasa na Uhusiano wa KIImataifa), wakiwapungia mikono wananchi wa Nyasa, baada ya kupanda Mv Songea katika bandari ndogo ya Mbamba Bay, kuanza safari ya kwenda Kyenla. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Nyasa, Ernest Kahindi 
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiagana na wananchi wa Mbamba Bay, Nyasa, kabla ya kupanda meli kwenda Kyela
 Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migirob akisalimiana na Nahodha wa Mv Songea Tom Faya, katika bandari ndogo ya Mbamba Bay, wilayani Nyasa mkoani Ruvuma kabla ya safari ya kwenada Kyela
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na Nahodha wa mv Songea, kabla ya safari ya kwenda Kyela kutoka bandari ndogo ya Mbamba Bay, Nyasa. Wapili kulia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Rukwa Oddo Mwisho
 Mkurugenzi na Mtayarishaji Mkuu wa theNkoromo Blog, Bashir Nkoromo, ambaye ni baadhi ya abiria walioko katika msafara wa Kinana,akipanda mv Songea.
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akipanda mv Songea. Wanaomfuata na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho na katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro.
 Wananchi na wanachama wa CCM wa Mbamba Bay, wilayani Nyasa mkoani Ruvuma, wakisindikiza kwa boti mv Songea wakati ikiondoka bandarini
Nahodha wa ,mv Songea na Kinana wakizungumza na waandishi wa habari. Imetayarishwa na theNkoromo Blog

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages