MKUU WA JESHI LA POLISI NCHINI |
POLISI mmoja na rais wawili wanadaiwa kufariki dunia watatu wengine kadhaa kujeruhiwa kufuatia vurugu ziulizosababishwa na mgogoro kati ya wakulima na wafugaji wa jamii ya kisukuma katika kijiji cha Igwati tarafa ya Malinyi wilayani Ulanga mkoani hapa.
Taarifa zilizopatikana kutoka eneo la tukio zimedai kuwa wakulima walivamia kituo cha polisi kwa lengo la kushinikiza wenzao watatu kuachiwa, baada ya kukamatwa wakituhumiwa kumuua mfugaji wa jamii ya kisukuma hivi karibu aliyetambulika kwajina la Matanyi Luchoma (16).
Imedaiwa kuwa wananachi hao baada ya kupata taarifa za kukamatwa kwa wenzao walifika kituo cha polisi ambapo, hawakuwakuta watuhumiwa hao baada ya polisi kuwahamishia kituo kingine na hivyo kuamua kuchoma moto kituo hicho pamoja na gari la jeshi hilo.
Wananchi hao walifanya vurugu kituoni ambapo , yalitokea mapiganokati yao na askari wa jeshi la polisi, hivyo kumuaa askari mmoja, na askari nao kuwaua wananachi wawili na kujeruhi wengine watatu.
Mtandao huu ulimtafuta Kamanda wapolisi mkoa wa Morogoro Faustine Shilogile ili kuthibitisha taarifa hizo ambapo simu zake zilikuwa hazipatikani .
Kaimu Kamanda wapolisi John Laswai alidai kuwa RPC yuko eneo la tukio na kukikiri kuwepo kwa tukio hilo, huku akidai kuwa hana taarifa za vifo hivyo kikiwemo cha askari huyo, na kumtaka mwandishi kuendelea kuwasiliana na Kamanda wa polisi aliye eneo la tukio .
Chanzo cha mgogoro huwa kinadaiwa kuanza Desemba 13 mwaka huu saa 2 usiku katika kijiji cha Igwati Malinyi Wilayani Ulanga kundi la wananchi lilimkamata mfugaji huyo mkazi wa Lupeleme na kumpelekakatika ofisi za kijiji cha Lugawa.
Ilidaiwa kuwa baada ya kumfikisha kwenye ofisi hizo, mtendaji alimfungia mtuhumiwa ofisini, na kuanza kuhoji sababau ya wananachi kujichukulia shera jambo ambalo halikuwapendeza hivyo kuanza kumshambulia mtendaji huo naye kukimbia na wao kuvunja ofisi na kumpiga kijana huyo na kusababaisha kifo chake.
Hata hivyo ilidaiwa kuwa chanzo cha mauaji hayo kilisababaishwa na baadhi ya watu wanaodawa kuwa wa wafugaji wa jamii ya kisukuma kuvamianyumbani kwa Mjumbe wakamati ya mazingira Victoria Marietha, kasha kumpiga na kumsababishia majeraha.
Mjumbe huyo alipelekwa haraka katika hospitali ya Lugala, Tarafa ya Malinyi ambapo alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu, na hivyo wakulima hao kuanza kuwasaka wafugaji wa jamii ya kisukuma.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269