Breaking News

Your Ad Spot

Feb 4, 2014

MAHMOUD THABIT KOMBO AAPISHWA KUWA MWAKILISHI MPYA KIEMBESAMAKI

 
 Msafara wa Mwakilishi Mpya wa Jimbo la Kiembesamaki ukiingia katika viwanja Baraza la Wawakilishi kumshindikiza kwa ajili ya kuapishwa leo asubuhi. 
 Gari iliomchukuwa Mhe. Mahmoud Thabit Kombo likingia katika viwanja vya Baraza leo asubuhi kwa ajili kuhudhuria kuapishwa na kushiriki katika Kikao cha Baraza la Wawakilishi kinachoendelea kujadili Ripoti za Kamati za Baraza Zinazowakilishwa na Wenywviti wa Kamati hizo.
 Mhe. Mwakilishi Mteule akiwasili katika viwanja vya Baraza la Wawakilishi Chukwani tayari kwa kuapishwa Rasmin kuwa Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki Zanzibar, akishindikizwa na Mwakilishi wa Jimbola Rahaleo Mhe Nassor Salim Jazira na katikati Mwakilishi wa Bububu Mhe Hussein Ibrahim Makungu (BHAA) wakimshindikiza katika ukumbi wa Mkutano kwa ajili kuapishwa
Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Yahya Khamis Hamad, akisalimiana na Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki Mhe. Mahmoud Thabit Kombo alipowasili katika Ofisi ya Katibu wa Baraza kwa ajili kujitambulisha na kuhudhuria kuapishwa kwake kuingia katika Baraza la Wawakilishi baada ya kushinda kiti hicho katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki uliofanyika wiki iliopita.
Mhe. Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Pandu Ameir Kificho akiingia katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi kwa ajili ya kuaza kwa taratibu za shughuli za Kikao na kumapisha Mwakilishi Mpya wa Jimbo la Kiembesamaki Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo. wakati wa Kikao cha asubuhi leo. 
Mhe. Spika Pandu Ameir Kificho akisoma Dua kabla ya kuaza kwa Kikao cha Baraza cha Asubuhi leo. 


Waheshimia wakisimama wakati wa kusomwa kwa dua kabla ya kuaza kwa Kikao cha Baraza. 
Wageni walioongozana na Mhe. Mahmoud Thabit Kombo wakisimama wakati wa kusomwa kwa Dua kabla ya kuaza kwa shughuli za Kikao cha Baraza leo asubuhi.
Wanafamilia ya Mhe. Mahmoud Thabit Kombo wakihudhuria sherehe za kuapishwa kwake leo asubuhi katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Waheshimiwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Wanawake wakimshindikiza Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akiingia katika ukumbi wa Mkutano tayari kwa kuapishwa kwake kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa Jimbo la Kiembesamaki Zanzibar baada ya kushinda nafasi hiyo katika uchaguzi mdogo uliofanyika mwishoni mwa wiki.
Waheshimiwa Wawakilishi wa Chama cha Mapinduzi wakimshangilia Mwakilishi wao wa Jimbo la Kiembesamaki wakati akiapishwa katika ukumbi wa Mkutanona Mhe. Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho leo asubuhi. 
Mhe Mhmoud Thaib Kombo, akiapishwa na Spika wa Baraza la Wawakilishi kuwa Mwakilishi wa Jimbola Kiembesamaki, baada ya kushinda Jimbo hilo na kuwa Mwakilishi Mpya kuchukua nafasi ya aliyekuwa mwakilishi wa jimbo hilo Mhe. Mansoor Yussuf Himid.    
Waheshimiwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakifuatilia kuapishwa kwa Mhe. Mahmoud Thaib Kombo, baada ya kushinda uchaguzi mdogo wa jimbo la kiembesamaki Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM. 
Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akitia saini baada ya kuapishwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Jimbo la Kiembesaki Zanzibar kwa kupata ushindi katika uchaguzi mdogo uliofanyika wiki iliopita.
Mhe. Spika wa Baraza la Mapinduzi Pandu Ameir Kificho akimkabidhi Vitendea Kazi vya Baraza la Wawakilishi Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo.baada ya kuapishwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi.




Mhe.Mahmoud Thabit Kombo akifurahi baada ya kuapishwa akiwa na Mwakilishi wa Bububu Mhe.Husein
Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akiwa katika picha ya pamoja na familia yake na Waheshimiwa wa Baraza nje ya Ukumbin wa Baraza la Wawakilishi baada ya kuapishwa.






Wananchi wa Jimbo la Kiembesamaki wakimshangilia Mwakilishi wao nje ya Majengo la Baraza la Wawakilishi.
Mhe. Mahmoud Thabi Kombo akiwashukuru wananchi wa jimbo la kiembesamaki kwa mashirikiano yao tangu mwazo wa kampeni hadi kupiga kura na kumchagua kuwa mwakilishi wao. 




Picha zote kwa hisani ya  mtandao wa http://www.zanzinews.com

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages