Breaking News

Your Ad Spot

Feb 21, 2014

MEMBE: TANZANIA KUENDELEA KUSAIDIA MASUALA YA AMANI BARANI AFRIKA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu masulala mbalimbali ya uhusiano wa kimataifa ikiwamo hatua zinazochukuliwa na Tanzania katika kusuluhisha Migogoro inayotokea ndani na nje ya mataifa mbalimbali na kusisitiza kuwa Tanzania haiwezi kuingia katika mgogoro na majirani zake, Wakati wa Mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe akifanya mahojiano na Mwandishi wa shirika la utangazaji la Uingereza (BBC) Erick David Nampesya leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa Habari waliohudhuria mkutano wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam. 

(Picha na Hassan Silayo)

Frank Mvungi
Serikali ya Tanzania imesema  haina ugomvi na nchi jirani kwa kuwa ni wadau  wa maendeleo katika  kujenga uchumi imara kwa kutumia fursa  zilizopo.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe wakati akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es salaam kuhusu taarifa mbalimbali zinazoripotiwa na vyombo vya habari kuhusu uhusiano wa Tanzania na Rwanda.

Akieleza zaidi Mh.Membe alisema vyombo vya habari  vinalojukumu kubwa la kuielimisha jamii na kuimarisha uhusiano kati Tanzania na nchi jirani na si kufanya jambo lolote linaloweza kuleta tofauti kati ya Taifa moja na jingine.
Mh. Membe amesema kuwa Tanzania ni nchi inayotumia njia za Kidiplomasia kuondoa tofauti zozote zitakazojitokeza  kati yake na nchi yoyote na haina mpango wa kuingia kwenye mgogoro na nchi yoyote ile.

Aliongeza kuwa Tanzania kwa miaka mingi imekuwa kisiwa cha amani na mfano bora katika bara la Afrika ndio maana imekuwa mstari wa mbele katika kutatua migogoro ndani ya bara la Afrika.

Akifafanua zaidi Mh. Membe amesema Tanzania imepeleka vikosi vyake  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,Lebanon,Sudan ya Kusini, katika kutimiza jukumu la kulinda amani Duniani.

“Tunafikri ni vyema Jukumu la ulinzi  wa Bara la Afrika likawa mikononi mwa Afrika yenyewe” alisisitiza Mh.Membe alipokuwa akifafanua kuhusu nafasi ya Tanzania katika kuleta amani katika mataifa mbalimbali ndani na nje ya Bara la Afrika.

Pia alieleza kuwa tangu harakati za ukombozi wa bara la Afrika Tanzania imekuwa  makao makuu ya vyama vyote vya ukombozi barani Afrika na kusaidia katika harakati za kuleta ukombozi .

Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa mwaka huu imepanga kufanya maandalizi mazuri yatakayoiwezesha timu ya Taifa kushiriki na kupata medani katika michezo ya jumuiya ya madola.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages