Breaking News

Your Ad Spot

Apr 6, 2014

RAIS KIKWETE, RIDHIWANI KIKWETE WAPIGA KURA LEO UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA CHALINZE

 Rais Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, akisoma fomu ya maelekezo kabla ya kupia kura, aliposhiriki kupiga kura kwenye kituo cha Zahanati ya Msoga, katika uchaguzi mdogo jimbo la Chalinze mkaoni Pwani, leo. Mgombea wa CCM katika kinyang'anyiro hicho ni mtoto wake, Ridhiwani Kikwete.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa kwenye chumba cha kupigia kura wakati wa kupiga kura za kumchagua Mbunge mpya wa Jimbo la Chalinze.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitumbikiza kura yake kwenye kisanduku.
 Mama Salma Kikwete akiweka kura yake kwenye kisanduku baada ya kupigia kura yake kwenye kituo cha Zahanati Msoga.
 Mgombea wa Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia Chama Cha AFP, Ramadhani Mgaya akizungumza na waandishi wa habarai nje ya kituo cha Ofisi ya Mtendaji Kata namba moja na kusema kuwa Chama chake kitakubali matokea yeyote na pia kama watashindwa watajipanga kwa ajili ya uchaguzi wa 2015.
 Mgombea wa Chadema katika uchaguzi huo, Mathayo Torongey akizungumza na baadhi ya mawakala alipotembelea kituo cha Ofisi Mtendaji Kata namba moja, Bwilingu.
 Ridhiwani akihakiki taarifa zake kabla ya kupiga kura kwenye kituo cha Ofisi ya Mtendaji Kata namba 3 Bwilingu, Chalinze.
Ridhiwani akimsaidia mwanae, Aziza Ridiwani, kuweka kura kwenye sanduku la kura baada ya kupiga kura yake kwenye uchaguzi huo katika kituo kilichopo kata ya Bwilingu.
Mkurugenzi wa Uchaguzi Jimbo la Chalinze Samuel Salianga akizungumza na waandishi wa habari nje ya kituo cha Ofisi ya Mtendaji Kata Bwilingu na kutoa tathmini ya jinsi zoezi linavyoendelea na kufafanua mambo mbali mbali yanayohusu uhalali wa wagombea kupiga kura popote ndani ya jimbo la uchaguzi.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages