Breaking News

Your Ad Spot

Apr 6, 2014

TPA YATOA MSAADA WA MADAWATI 110 SHULE YA MSINGI MAHUMBIKA MKAONI LINDI

Mkuu wa Bandari ya Mtwara, Absalom Bohela (kushoto) akikabidhi msaada wa madawati 110 yenye thamani ya shilingi milioni 20 kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mh. Ludovick Mwananzila (kulia) wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika hivi karibuni katika kijiji cha Mahumbika kilichopo Lindi vijijini.

 Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mh. Ludovick Mwananzila (kulia) na Mkuu wa Bandari ya Mtwara, Absalom Bohela (kushoto) wakiwa na baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Mahumbika wakati wa kukabidhi msaada wa madawati 110 yenye thamani ya shilingi milioni 20 kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), kwa shule za mkoa wa Lindi hivi karibuni.



Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Dkt.  Hemid Nassoro akizungumza na wakazi wa kijiji cha Mahumbika kabla ya kupokea msaada wa madawati 110 yenye thamani ya shilingi milioni 20 kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), kwa shule za mkoa wa Lindi hivi karibuni.

Mkuu wa Bandari ya Mtwara, Absalom Bohela akisoma hotuba kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kabla ya kukabidhi msaada wa madawati 110 yenye thamani ya shilingi milioni 20 kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mh. Ludovick Mwananzila hivi karibuni.
 Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Mahumbika wakifurahia jambo wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa madawati 110 yenye thamani ya shilingi milioni 20 kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), iliyofanyika hivi karibuni katika kijiji cha Mahumbika kilichopo Lindi vijijini.



Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Mahumbika wakiimba wimbo wa Taifa wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa madawati 110 yenye thamani ya shilingi milioni 20 kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), iliyofanyika hivi karibuni katika kijiji cha Mahumbika kilichopo Lindi vijijini.



Wasanii wa kikundi cha ngoma na maigizo cha kijiji cha Mahumbika, Lindi wakitoa burudani wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa madawati 110 yenye thamani ya shilingi milioni 20 kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), iliyofanyika hivi karibuni katika kijiji cha Mahumbika kilichopo Lindi vijijini.


No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages