Breaking News

Your Ad Spot

May 27, 2014

Picha na Taarifa Kutoka Afisa Habari Mkoa wa Tanga:Mkoa wa Tanga watunukiwa tuzo kwa kufanya vizuri katika Sekta ya Elimu Nchini.

    Picha ya Tuzo iliyopokea mkoa wa Tanga wakati wa maadhimisho ya wiki ya Elimu Tanzania, “Hongera Mkoa waTanga”.
     Mkuu wa Mkoa wa Tanga Chiku Gallawa (kulia) akipokea tuzo ya mkoa wake kufanya vizuri 2013 katika sekta ya Elimu kutoka kwa Katibu Tawala wa Mkoa huo  Salum Mohamed Chima (kushoto) hivi karibuni ofisini jijini Tanga. Tuzo hiyo ilikabidhiwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda, wakati wa sherehe za uzinduzi wa wiki ya Elimu nchi niiliofanyika mapema mwezi Mei 2014 mjini Dodoma ambapo mkoa wa Tanga umekuwa wa kwanza kitaifa kwa kuwa na shule nyingi zililizofanya vizuri katika mitihani  ya Taifa ya Darasa la Saba, kidato cha nne na Kidato cha sita kwa mwaka 2013.
  Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Chiku Gallawa(kushoto) akimpongeza Katibu Tawala Msaidizi upande wa Elimu Mkoa Ramadhani Chomola (kulia).
KatibuTawala Mkoawa Tanga Salum Mohamed Chima (kushoto) akikabidhiwa Tuzo ya elimu ya mkoa na Katibu Tawala Msaidizi upande wa Elimu Ramadhani  Chomola mara baada ya kuiwasilisha kutoka Dodoma. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Chiku Gallawa.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages