Breaking News

Your Ad Spot

May 27, 2014

Waziri wa Habari Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara amewatumia salamu za rambirambi waandishi wa habari kufuatia kifo cha Mpiga picha wa kituo cha television cha Mlimani, Ndugu Maximilian John kilichotokea alfajiri ya kuamkia Jumamosi wiki iliyopita.


 Waziri wa Habari Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara 
---
 
Waziri wa Habari Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara amewatumia salamu za rambirambi waandishi wa habari kufuatia kifo cha Mpiga picha wa kituo cha television cha Mlimani, Ndugu Maximilian John kilichotokea alfajiri ya kuamkia Jumamosi wiki iliyopita.

Dkt. Mukangara amesema amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Bwana Maximilian kilichotokana na maradhi ya Moyo, Sukari  na Shinikizo la damu na ameongeza kuwa kifo hicho ni pigo na pengo kubwa kwa tasnia ya habari hapa nchini.

Amesema Bw. Maximilian atakumbukwa kwa uchapakazi na uhodori wake wa kazi zake uliokuwa unazingatia weledi wa taaluma ya uandishi wa habari, jambo lililomfanya awe na marafiki wengi wa tasnia hiyo.

Nakutumia salamu zangu za dhati kuomboleza msiba huu mkubwa kwa watumishi wote wa Mlimani TV, tasnia ya habari na familia yake kwa ujumla, amesema Dkt. Mukangara.  
Ameongeza kuwa Bw. Maximilia atakumbukwa daima na waandishi wa habari na wadau wengine kwa ucheshi wake,ushirikiano na wenzake wakati wa kutekeleza majukumu ya kitaalum na ujenzi wa Taifa kupitia Sekta ya habari.

 “Ninaungana na waandishi wa habari na wadau wengine katika kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, aiweke peponi roho ya marehemu. Amen,” amesema Dkt.Mukangara.

Imetolewa na;
IDARA YA HABARI, VIJANA , UTAMADUNI NA MICHEZO
26 Mei, 2014

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages