William Mhando akiingia katika chumba cha
Mahakama.
Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu
wa TANESCO, William Mhando (kushoto) akitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu jijini Dar es Salaam Jana , ambapo alisomewa shitaka la matumizi mabaya ya
madaraka
---
Na Happines Katabazi
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(TAKUKURU), ilimfikisha Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Da es Salaam jana ,
aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme(TANESCO), William Mhando na Mkewe
Eva Mhando pamoja na maofisa wengine wa serikali makosa mbalimbali likiwemo
kosa la matumizi Mabaya ya madaraka na kughushi.
Mbali na Mhando na Mkewe ambao wanatetewa na wakili wa kujitegemea Jamhuri Johnson, washitakiwa wengine ni Francis Machalange ambaye ni Mhasibu Mkuu wa Tanesco,Sophia Misidai ambaye ni Mhasibu Mkuu na Naftali Kisinga ambaye ni Ofisa Ugavi wa Shirika Hilo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269