Breaking News

Your Ad Spot

Nov 15, 2014

MAKAMU WA RAIS DK.MOHAMMED GHARIB BILAL AFUNGUA MKUTANO WA VIONGOZI WA CHAMA CHA MAPINDUZI MKOA WA DAR ES SALAAM WA KUJADILI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA NA UCHAGUZI MKUU WA 2015 UKUMBI WA KARIMJEE DAR ES SALAAM LEO

Makamu wa Rais na Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akitoa hutuba kwa viongozi wa CCM mkoa wa Dar es Salaam leo.
Makamu wa Rais na Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Dk. Mohamed Gharib Bilal (kulia) na Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida wakiingia ukumbi wa Karimjee kwa ajili ya mkutano. (Imeandaliwa na www. habari za jamii.com)

viongozi mbalimbali wa chama hicho kuanzia ngazi ya chini wakiwemo wajumbe wa Halmashauri Kuu za Wilaya na Mkoa wakimkaribisha mgeni rasmi wa mkutano huo, Makamu wa Rais Dk.Mohamed Garib Bilal (hayupo pichani)
Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba "Gadafi" akizungumza katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida, akihutubia kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Makamu wa Rais Dk. Bilal.
Makamu wa Rais ambaye pia ni mlezi wa Chama Cha Mpinduzi Mkoa wa Dar es Salaam Dk. Mohamed Gharib Bilal (katikati), akizungumza na viongozi wa CCM mkoa wa Dar es Salaam leo, kuhusu uchaguzi wa Serikali za Mitaa na uchaguzi mkuu 2015. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida.

Viongozi mbalimbali wa CCM wakiwa kwenye mkutano huo.
Diwani wa Kata ya Kipawa, Bonah Kaluwa (katikati), akifurahia jambo na viongozi wenzake katika mkutano huo.

Viongozi mbalimbali wa CCM wakiwa kwenye mkutano huo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Wanaccm wakiwa wamefurika ukumbi wa Karimjee 
katika mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.

Wanaccm wakiwa katika mkutano huo.

Dotto Mwaibale

MAKAMU wa Rais ambaye pia ni mlezi wa Chama Cha Mpinduzi Mkoa wa Dar es Salaam Dk. Mohamed Gharib Bilal ametoa mwito kwa viongozi na wanachama wa chama hicho kuacha misuguano na mifarakano ili kukiepusha chama hicho na mipasuko isiyo ya lazima.


Dk. Bilal alitoa mwito huo Dar es Salaam leo asubuhi wakati akiwahutubia katika mkutano uliowakutananisha viongozi mbalimbali wa chama hicho kuanzia ngazi ya chini wakiwemo wajumbe wa Halmashauri Kuu za Wilaya na Mkoa kujadili uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa 2015.

Alisema CCM ni chama pekee hapa nchini ambacho kinafanya shughuli zake kidemokrasia na ndio maana kinaendelea kushika dola na kukubalika na wananchi.

Dk.Bilal alisema  katika kipindi hiki cha mchakato wa kuwapata viongozi kuelekea katika chaguzi mbalimbali kunakuwa na changamoto za hapa na pale hivyo wenye dhamana ya kuwateua wagombea wanapaswa kutenda haki kwa kumteua yule aliyepigiwa kura kwa wingi badala ya kufanya ndivyo sivyo.

"Chama Cha  Mapinduzi ndio chama chenye dira na sera zinazotambulika hivyo viongozi wake wanapaswa kuwa makini na kuhakikisha hakuna makundi yanayoweza kuwagawa wanachama" alisema Bilal


Alisema  viongozi wa chama hicho  wana wajibu mkubwa wa kuhakikisha chama hicho kinapata ushindi wa kishindo katika chaguzi zote kwani uwezo wa kufanya hivyo upo kwa kuwa chama hicho kimejipanga vizuri kuanzia ngazi ya shina na kina maadili.


Bilal aliongeza kuwa kila uchaguzi unapofanyika watu na vyama vingine wanaangalia CCM imemsimamisha nani hivyo ni vizuri wakati wa uteuzi wa viongozi wanapaswa kuwa makini kwa kumchagua aliyebora.


Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida alisema wamejifunza mengi katika chaguzi zilizopita ambapo walipoteza maeneo kadhaa kwa kuchuliwa na vyama v, kwa sasa wako katika hatua za mwisho za kupata mgingine kutokana na makosa hayo.

Alisema hivi sasa mwanachama yeyote atakaye shinda kura za maoni ndiye atakayekuwa mgombea katika eneo husika labda tu awe amepita kwa rushwa na mambo mengine ambayo yatathibishwa.

Madabida alisema kwamba katika mchakato wa kuwapata wagombea wa nafasi za serikali za mitaa kulikuwa na changamoto za hapa na pale ambazo watahakikisha zinafanyiwa kazi ili mambo yaende sawa.
 (Imeandaliwa na www. habari za jamii.com)

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages