Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya
Obi Mobiles, Bw Amit Rupchandani (kati kati) wakionyesha simu mpya aina
ya Obi Mobiles kwenye uzinduzi rasmi wa simu hizo jijini Dar es
Salaam.Kulia ni Farouk Jivani kutoka kampuni ya Direct Specialist na
Kushoto ni Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Obi Mobiles, Yusuf Kamal
Khan .
………………………………………………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu
Mwanzilishi wa Obi Mobiles na
Mkurugenzi Mtendaji wa zamani Apple, John Sculley aahidi utendaji wenye
tija katika vifaa vya simu za mkononi chini ya nembo ya Obi nchini.
Kampuni ya Obi Mobiles inalenga kuongeza mauzo kupitia mpango mkakati unaowalenga vijana na walaji wengine
kupitia aina mbalimbali ya simu ambayo itakuza upatikanaji wa
mtandao na kufanya Tanzania moja ya nchi bora katika upatikanaji wa
teknolojia ya mawasiliano.
Tanzania: Februari 24, 2015 – Obi Mobiles, Simu yenye teknolojia
mpya na nembo ya Mwanzilishi na Mkongwe katika mambo ya Masoko na
Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa Apple, John Sculley, ni mbia mpya
katika kampuni ya Inflexionpoint yenye makao makuu Sculley’s Toronto,
Nembo hii mpya ya kampuni ilifanya uzinduzi wake mkubwa nchini India na
Mashariki ya Kati mwaka 2014.
Walengwa wakubwa katika kampuni hii ni vijana na watu
wanaokwenda na wakati wa matumizi ya simu za mkononi, Simu na vifaa vya
Obi vimepokelewa kwa hamasa kubwa katika masoko na simu ina matumaini
wataendelea kupata wateja wengi siku za usoni.
Kampuni ya Obi Mobiles ilizindua aina saba za simu mbalimbali
kwa ajili ya soko la Tanzania. Aina hizo za simu ni kama vile Hornbill
S551 kwa TSh 350,000, Falcon S451 TSh 290,000, Crane S550 TSh 270,000,
Wolverine S501 TSh220,000, Fox S453 TSh160,000, Racoon S401 TSh 130,000
na Power GO F240 – simu yenye uwezo mkubwa na vipengele mbalimbali
2,800mAH betri, na ina Power Bank (chaji benki) yenye uwezo wa kuchaji
simu nyingine TSh 50,000.
Imani ya msingi katika kampuni ya Obi Mobiles ni kwamba
teknolojia ni kitu cha lazima kwa kila mtu na uunganishwaji ni fursa ya
kufungua mianya ya nafasi za biashara na kusaidia kukua kiuchumi na
maendeleo ya kijami.
kwa taifa husika. Maono ya John
Sculley ni kuhakikisha kwamba teknolojia isiwe kikwazo kwa mtu yeyote
kupata kutokana na matatizo ya kimtandao au vikwazo vyovyote ambavyo
vitasababisha watu wengi zaidi kukosa fursa hii.
Smartphones mpya za Android zilizozinduliwa na Obi Mobiles hutoa
huduma bora zaidi na teknolojia ya hali ya juu na kwa mantiki hiyo
kutoa fursa kwa watumiaji wa Tanzania kuwa katika nafasi nzuri zaidi ya
kufurahi intaneti kupitia uzinduzi wa simu hizo saba tofauti tofauti,
uzinduzi rasmi wa simu hii kutoka kampuni ya Obi ni Mwezi Machi tarehe
7.
Akizungumza juu ya mkakati wa kampuni hiyo Afrika, Mkurugenzi
Mtendaji wa Obi Mobiles MENA, Amit Rupchandani, alisema: “Wateja
wanaongezeka kwa kuangalia jinsi ya kuboresha matumizi ya simu zao za
mkononi kutoka katika simu za zamani kwenda kwenye simu za
(smartphones). Hata hivyo, gharama kubwa za uwekezaji katika vifaa ya
simu hizi mpya- na umri wa simu hizi mpya na matamanio ya wanunuzi wapya
ni wakati mwafaka kwa kampuni ya Obi Mobiles, ambao tunaamini kutia
alama ya vema katika box hili jipya katika maswala ya ubora wa simu, bei
ili kuweza kuwafikia kila aina ya mteja katika soko ili kuongeza
thamani katika soko la simu bara la Afrika,”
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269