Mbunge wa Mbinga Magharibi Mh. Kapteni John Komba amefariki Dunia leo saa 10 jioni katika Hosptali ya TMJ Mikocheni.
Kwa
Mujibu wa mtoto wa Marehemu Bw. Jerry Komba amesema kifo cha marehemu
baba yake kimetokana na ugonjwa wa kisukari ambapo amedai kuwa sukari
ilishuka ghafla akiwa nyumbani kwake Mbezi Beach Dar es salaam.
"Ni kweli mzee amefariki dakika 50 zilizopita, alikuwa nyumbani amekaa
lakini sukari ilishuka ghafla na baadaye kidogo alifariki" amesema Jerry
Komba mtoto wa marehemu.
Katibu wa mbunge huyo Bwana Gasper Tumaini amesema kuwa mbunge huyo
alikimbizwa katika hospitali ya TMJ ambapo ndipo mauti yamemkuta.
Aidha Bwana Gaspaer Tumaini ameongeza kuwa mwili wa marehemu umehamishiwa katika hosptali ya Lugalo jijini
Dar es salaam ambapo ratiba ya Mazishi bado haijafahamika.
Eatv imewatafuta Afisa habari wa Ofisi ya Bunge ndugu Owen Mwandumbya,
Mkurugenzi wa Mambo ya nje na Elimu kwa umma bwana Jesse Mwakasyuka na
katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashilila bila mafanikio kwa kuwa hawakupokea
simu
“mwenyezimungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269