WANANCHI WA KATA YA MASOKO WILAYA YA RUNGWE MKOANI MBEYA HAWATAKI PIGA KURA ZA MAONI YA KATIBA MPYA NA UCHAGUZI MKUU KUTOKANA NA KUTOKAMILIKA KWA MRADI WA MAJI WA MASOKO
Wananchi
wa kata ya masoko wilayani Rungwe mkoa wa Mbeya wamesema hawatopiga
kura ya maoni ya rasim ya katiba na kwa kuipigia kura ccm kwa kushindwa
kutekeleza mradi wa maji wa masoko ulioanza kutekelezwa tangu mwaka
2012 mpaka sasa mwaka 2015 haujakamilika.
Akiongea
kwa niaba ya wananchi diwani wa kata ya kisiba bwana Samweli Mwakyusa
kupitia chama cha Mapinduzi amesema kwamba mradi huo wa maji
umeshusha hadhi ya chama cha CCM kwa kuwa mradiwa maji umegubikwa na
utekelezaji mbovu na siasa zinazopelekea viongozi wa serikali na chama
kutokuwa waaminifu katika kutekeleza mradi huo na mpaka sasa wananchi
kukosa maji.
Wakiongea
wananchi mbele ya kamati ya maji kilimo na mifugo iliyongozwa na
mwenyekiti wa kamati Prf. Peter Kusolwa kiwemo mbunge wa Rungwe
magharibi Prf. David Mwakyusa mzaliwa wa kata hiyo ya masoko ambako
mradi wa maji unatekelezwa, wananchi wanashangaa kuona hata mbunge wao
hajawasaidia huku mkuu wa wilaya Crispin Meela akifanya ziara nyingi
zisizo na mafanikio katika mradi huo wa masoko .
Kamati
ya Bunge ya maji kilimo na mifugo ikiongozwa na mwenye kiti wa
kamati prf. Peter kusolwa na kuongozana na mbunge wa Rungwe
magharibi na kupokelewa na mkuu wa wilaya, makamu wa halmashauri
ya Rungwe na busokelo na viongozi wa maji mkoa wa Mbeya na
Tukuyu. imetembelea na kukagua miradi ya maji wirayani Rungwe, miradi
iliyotembelewa ni mradi wa kijiji cha itete na Kapugi na mradi wa
masoko.
Kabla
ya kukagua miradi hiyo mkuu wa wilaya alikabidhi ripoti za miradi hiyo
na kuelezea changamoto walizokumbana nazo kuwa ni kukosa wataaram wa
maji, na madeni ambayo yamepelekea kutomalizika kwa baadhi ya miradi.
Hivyo alishauri serikali kuanzisha wakara wa miradi ya maji vijijini
kwani hii itawasaidia kupambana na changamoto zinazowakabiri
na ameitaka wizara ya maji kuiga mbinu zinazofanywa na wizara ya miundo
mbinu ili kukamilisha miradi mikubwa ambayo haijakamilika.
Nae
makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Rungwe diwani Ezekiel mwakota
amesema kwamba tatizo ni mtiririko wa fedha na ndio chanzo cha
kutomalizika kwa miradi mbalimbali. Na mradi uliokwama ni mradi wa
masoko na ni kutokana na kukosa fedha za kuendelezea mradi huo.
Wakazi
wa kijiji cha Itete na Kapugi wameipongeza serikari kwa kufanikisha
mradi wa maji wa Kapugi na Itete na wameomba kuongezewa mpira
utakoakuwa unatoa maji kutoka chanzo kwenda kijiji cha Itete na Kapugi
kwani bomba la mpira lililopopo linatumika na vijiji vitatu kikiwemo
kijiji cha kyimo na halmashauri tayari inampango wa kutoa mpira wa nchi
tatu utakao peleka maji katika vijij vilivyoomba bomba hilo.
Kamati
ya maji kilimo na ufugaji imedai kushughurikia matatizo hayo na
kuwashauri wananchi kuunda kamati ya maji itakayosimamia miradi hiyo na
kutunza mazingira ili kutunza vyanzo vya maji kwani vitawakomboa
wasitembee umbali mrefu wakitafuta maji na wamewaasa kuchemsha maji ya
kunywa kuepukana magonjwa ya matumbo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269