Breaking News

Your Ad Spot

Feb 27, 2015

WATU 3 WAMEFARIKI DUNIA KWA KUUNGUA NA MOTO HADI KUTEKETEA KABISA AKIWEMO DEREVA NA UTINGO WAKE

 
Watu watatu wamefariki dunia kwa kuungua moto hadi kuteketea kabisa akiwemo dereva na utingo wake baada ya lori la mafuta kuacha njia na kupinduka na kuungua moto katika eneo la Maseyu barabara ya Morogoro Dar es Salaam.
Kikosi cha zimamoto walichukua muda kuuzima moto huo kutokana na kusambaa ambapo hata hivyo hakukua na matukio ya watu kujitokeza kuiba mafuta kama ilivyozoeleka.
Baada ya kumaliza kuuzima moto huo kikosi cha zimamoto na uokoaji wakafanya juhudi nyingine za kuvuta kwa craine na kukata kwa kutumia mashoka mabaki ya lori hilo baada ya walioshuhudia tukio hilo kueleza kuwa watu wote waliokuwemo katika gari hawakutoka ambapo baada ya muda miili mitatu iliokolewa ikiwa imeungua kabisa.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wakiwemo madereva wa malori ambapo walikuwa wakisafirisha mafuta katika kampuni moja Farhan Yusufu amesema lori hilo lilikua limesheheni mafuta ya Dezel mali ya kampuni ya Petrol Africa ilikua ikitokea Dar es salaam kwenda jijini Mwanza ambapo ilipoteza uelekeo na kupinduka kisha kuwaka moto.
Waliofariki dunia ni Ahmed Dilie dereva na utingo wake aliyefahamika kwa majina ya Emela na mtu mmoja ambaye bado hajaweza kufahamika mara moja.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages