Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiifajiri Familia ya
Sheha wa Shehia wa Kibweni Bibi Asha Ali Nassor ambayo moja ya chumba
cha nyumba hiyo kimeteketea na kuunguza vitu vyote vilivyokuwemo. Kulia ya Balozi Seif ni Mkuu wa Wilaya ya Magharibi Nd. Ayoub Mohammed Mahmoud.
Balozi
Seif akikagua hasara iliyotokana na moto katika chumba cha Nyumba ya
Sheha wa Kibweni Bibi Asha Ali Nassor Wilaya na Magharibi Mkoa wa Mjini
Magharibi. Kushoto
kwa Balozi Seif ni Mkuu wa Wilaya ya Magharibi Nd. Ayoub Moh’d Mahmoud
na kulia ya Balozi Seif ni Mmoja wa miongoni mwa wakaazi wa Nyumba hiyo
Bwana Abdulla Kombo Hamad.
Mtoto
wa Sheha wa Shehia ya Kibweni anayeishi ndani ya chumba kilichoteketea
kwa Moto Bibi Asumini Moh’d Juma akimueleza Balozi Seif mkasa ulimpata
kutokana na maafa hayo ya moto. (Picha zote na Hassan Issa–OMPR – ZNZ)
Na thman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
10/3/2015.
MAKAMU
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewashukuru na
kuwapongeza Wananchi wa Mtaa wa Kibweni Wilaya ya Magharibi kwa moyo
wao waliouonyesha katika kusaidia kuuzima moto ulioibuka majira ya saab
7.00 usiku juzi kwenye nyumba ya Sheha wa Shehia ya Kibweni Bibi Asha
Ali Nassor.
Alisema
licha ya kwamba vitu vyote vilivyokuwemo ndani ya chumba cha mmoja wa
watoto wa Sheha huyo alitwae Asumini Moh’d Juma kuteketea kwa moto huo
lakini juhudi za pamoja kati ya wakaazi wa nyumba hiyo na wananchi
jirani zimesaidia kuepuka maafa zaidi katika janga hilo.
Balozi
Seif Ali Iddi alisema hayo wakati alipofika Kibweni kuwafariji wakaazi
wa nyumba hiyo na kuwapa mkono wa pole kutokana na maafa hayo
akiambatana na Mkuu wa Wilaya ya Magharibi Nd. Ayoub Moh’d Mahmoud.
Alishauri
na kuomba mpango huo uendelezwe zaidi ili kutoa faraja kwa wananchi
wanaopatwa na maafa katika matukio mbali mbali yakiwemo yale ya moto na
hata ya tabia nchi.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar alimtaka mpatwa na maafa hayo Bibi Asumini
Moh’d Juma kuwa na moyo wa subira katika kipindi hichi cha mtihani na
kumtakia hali ya utulivu katika maisha yake ya baadaye.
Mapema
Mmmoja wa mashuhuda ya tukio hilo anayeishi ndani ya nyumba hiyo
Abdulla Kombo Hamad alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi
Seif kwamba moshi mkubwa uliotanda ndani ya nyumba hiyo ndio chanzo
kilichowatanabahisha kuwepo kwa hali isiyo ya kawaida vyumbani humo.
Abdullah
Kombo alisema wakazi wa nyumba hiyo kwa kusaidiana na majirani
walilazimika kuvunja mlango wa Chumba kilichokuwa na moshi mwingi cha
Bibi Asumini ambaye kwa wakati huo alikuwa Harusini na kufanikiwa
kuuzima moto huo.
Alifahamisha
kwamba baada ya kuangalia kwa kina chanzo cha moto huo walichodhania
kuwa ni hitilafu za umeme, wakagundua kuwa ni chupa ya mafuta ya
Petroli iliyopenyezwa kwenye durisha la nyuma la chumba hicho.
Abdullah
Kombo Hamad alielezea faraja yake baada ya kuona juhudi zao pamoja na
majirani zilisaidia kuudhibiti moto huo usiathiri mfumo wa waya za
umeme zilizomo ndani ya nyumba hiyo.
Naye
Mkaazi wa chumba hicho Bibi Asumini Moh’d Juma alisema kwamba moto huo
umesababisha kuteketeza vitu vyote vilivyokuwa vimehifadhiwa ndani ya
chumba chake.
Bibi
Asumini alivitaja baadhi ya vitu vilivyokuwemo ndani ya chumba chake
kuwa ni pamoja na kabati lililohifadhiwa nguo zote, Kitanda na Godoro
lake,Charahani, vyakula pamoja na baadhi ya vitu vya ndani.
Alisema
licha ya mtihani huo lakini anawashukuru watu wa wasamaria mbali mbali
kwa moyo wao wa huruma waliomuonyesha wa kumpatia baadhi ya huduma
zikiwemo nguo za kujistiri hali iliyompa faraja kubwa.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269