Na Mwandishi Maalum.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban ki Moon, amesema kama si utashi wa kisiasa, kujituma, na kujitolea kulikofanywa na viongozi mbalimbali aliowaomba kufanya naye kazi kwa karibu huku wengine wakijitolea wenyewe, uhai wa wanawake na watoto 2.4 milioni usingeokolewa.
Ban Ki Moon ameyasema hayo siku ya Jummane wakati wa uzinduzi wa ripoti mpya kuhusu mkakati wa kimataifa kuhusu vuguvugu la kila mwananamke, kile mtoto, ( every woman, every child) mkakati ambao Ban Ki Moon aliuratibu mwaka 2010 .
“ Siri kubwa ya mafanikio ya mkakati huu ni uwajibikaji. Nilipoanzisha mkakati huu niliwaomba baadhi ya viongozi wanisaidie, wapo waliosaidia katika uhamasishaji wa raslimali fedha, wapo kama Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania na waziri Mkuu wa Canada ambao walisimamia suala zima la habari na uwajibikaji, mchango wao, kujituma kwao na uthubutu wao ndiyo umetufikisha hapa , tumeweza kuokoa maisha ya wanawake na watoto wengi na kazi bado inaendelea” ameeleza Katibu Mkuu.
Akasema mkakati huo aliouzisha wa kila mwanamke, kila mtoto na ambao chimbuko lake ni lengo namba nne na tano la maendeleo ya millennia ni mkakati ambao si tu umekuwa wa mafanikio makubwa lakini umegusa hisia za wadau mbalimbali za watu wengi .
Malengo namba nne na tano ya maendeleo ya millennia na ambayo yanafikia ukingoni mwisho mwa mwaka huu yanajikita katika kupunguza idaidi ya vifo vya wanawake na idadi ya vifo vya watoto chini ya miaka mitano.
“Nilianzisha mkakati huu kwa sababu mimi mwenyewe nimeguswa katika maisha yangu utoto wangu kwa kuondokewa( kufariki) kwa kaka na dada zangu kwa matatizo ambayo yangeweza kuzuilika. Simulizi alizokuwa akisimuliwa na mama yake juu hofu kuu wanayokuwa nayo wanawake wanapokwenda kujifungua vile vile ni moja ya hamasa iliyonifanya nianzishe mkakati huu. Lakini pia katika utekelezaji wa majukumu yangu nimekutana na visa vingi vilivyoongeza nia na ari kuwa na mkakati huu” ameeleza Ban Ki Moon.
Ripoti hiyo ambayo uzinduzi wake umekwenda sambamba na mkutano wa 59 wa Kamisheni kuhusu hadhi ya wanawake, inabainisha kwa kina mafanikio na changamoto mbalimbali za utekelezaji katika eneo hilo linalohusu afya ya mama na mtoto.
Ban Ki Moon amesema amefarijika na kutiwa moyo sana.
Kwa mfano Makati huo ambao umegusa hisia wa wadu mbalimali wakiwamo viongozi wakuu wan chi na serikali, asasi zisizo za kiraia, wanaharakati na makampuni binafsi.
taarif yasingeushirikiano wa karibu baina yake na Viongozi wakuu wa mataifa mbalimbali umesaidia kuokoa maisha ya .., ambao wangepoteza maisha yao wakati wa kujifungua.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon akizungumza siku ya Jumanne, wakati wa uzinduzi wa ripoti mpya kuhusu mkakati wa kimataifa wa kila mwanamke, kila mtoto ambao Ban Ki Moon aliuanzisha mwaka 2010. Ripoti hiyo inaonyesha kuwa vuguvugu hilo ambalo kwa ushirikiano baina ya wadau mbalimbali zikiwamo serikali, mashirika ya kimataifa, asasi zisizo za kiserikali, wasomi, wanaharakati na sekta binafsi zimewezesha kuokoa maisha ya wanawake na watoto 2.4 milioni.
Your Ad Spot
Mar 11, 2015
Home
Unlabelled
BAN KI MOON AMFAGILIA RAIS JAKAYA KIKWETE
BAN KI MOON AMFAGILIA RAIS JAKAYA KIKWETE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269