Breaking News

Your Ad Spot

Mar 13, 2015

KINANA AMALIZA ZIARA YAKE DODOMA, DIWANI ALHAJI OMARI KARIATI AFANYA MAKUBWA KWADELO

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Sabasaba mjini Kondoa akiwa kwenye ziara ya kikazi wilayani humo, Kinana amemaliza ziara katika mkoa wa Dodoma yenye lengo la kukagua miradi ya maendeleo na inayotekelezwa na serikali na kuhimiza uhai wa chama cha Mapinduzi ambapo kesho anaendelea  ziara hiyo mkoani Arusha akianzia wilaya ya Monduli akiongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Ndugu Nape Nnauye.
Awali katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana ilikuwa asiende katika kata ya Kwadelo ambapo ratiba ya kwenda huko ilikuwa imeahirishwa lakini wakati Kinana akizungumza na wajumbe wa Mkutano mkuu wa wilaya ya Kondoa ndipo Diwania wa kata ya Kwadelo  Alhaji Omari Kariati alipomuomba Katibu Mkuu wa CCM kutumia busara zake na hekina na kuangalia kama anaweza kufika kata ya Kwadelo pia kwani wana CCM wa kata hiyo wana hamu kubwa ya kumuona na kuna miradi mingi ambayo angeweza kuitembelea na kuzindua ofisi ya CCM ya kata hiyo ambayo imejengwa  kwa ufadhili wa diwani huyo.
Ndipo Kinana alipokubali ombi hilo na kwenda kufanya ziara katika kata ya  Kwadelo pia ambako amejionea miradi kadhaa ikiwemo  ofisi ya CCM kata ya Kwadelo ambayo ameizindua na kukabidhiwa hati ya umiliki na diwani huyo na mradi wa matrekta yanayofanya kazi ya kilimo katika kata hiyo.
Akisoma taarifa yake mbele ya umati wa wananchi waliokuwa wakimshangilia Alhaji Omari Kariati, Amesema “Ahadi zake zilikuwa ni miradi 13 ambayo yote imekamilika kwa asilimia 100% na miradi mingine ambayo haikuwemo katika ahadi pia inaendelea kutekelezwa, Baadhi ya miradi ambayo imekamilika  ni Maji, Umeme, Mradi wa Matrekta  ya kilimo, Huduma za Afya na mingine mingi.
Baadhi ya wananchi waliofika kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Sabasaba mjini Kondoa. 3 
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akiwahutubia maelfu ya wananchi waliojitokeza katika mkutano wa hadhara mjini Kondoa. 4 
Baadhi ya wazee wa Kata ya Kwadelo wakimsikiliza katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana hayupo pichani. 10 
Baadhi ya wananchi wakinyoosha mikono yao juu kuashiria kukubali hotuba ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana. 11 
Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mh. Chiku Galawa akiwasalimia wananchi waliojitokeza katika mapokezi ya kinana. 14 
Wananchi wakiwa wamejitokeza kwa wingi kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM katika kijiji cha Itaswi. 15 
Mbunge wa jimbo la Kondoa Mh. Zubain Muhaji Mhita akizungumza na wananchi katika kijiji cha Changaa wilayani Kondoa wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipotemlbelea ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho. 16 
Mkuu wa wilaya ya Kondoa Mh. Shaaban Kisu akiwasalimia  wananchi katika kijiji cha Changaa. 17 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki katika kazi za mikono wakati alipotembelea kiwanda cha kukamua mafuta ya Alizeti mjini Kondoa.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages