Breaking News

Your Ad Spot

Mar 27, 2015

WAKUU WA MAJESHI YA ULINZI WAKUTANA UMOJA WA MATAIFA

 .Mkuu wa  Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange akiwa na,  kutoka kushoto,  Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi na kulia kwake,  Balozi Ramadhan Mwinyi, Naibu Mwakilishi wa Kudumu,  Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi  yupo hapa Jijini New York ambako atahudhuria na kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Majeshi ya Ulinzi ambao nchi zao zinatoa wanajeshi au polisi katika operesheni za ulinzi wa amani  chini ya Umoja wa Mataifa
 Mkuu wa  Majeshi ya Ulinzi na ujumbe wake  katika picha ya   pamoja na Mabalozi Tuvako  Manongi na  Ramadhan Mwinyi.
Maafisa wa Uwakilishi wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa wakiwa katika picha ya pamoja na  Mkuu wa  Majeshi ya Ulinzi, pamoja na Mabalozi.

HABARI KAMILI
 Na Mwandishi Maalum, New  York
Wakuu wa Majeshi ya Ulinzi ambao nchi zao zinachangia wanajeshi    au Polisi  katika operesheni za kulinda Amani chini ya Umoja wa Mataifa,  wanakutana hapa  Makao Makuu ya  Umoja  wa Mataifa  katika mkutano unaoelezwa kuwa wa kihistoria.
 Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jenerali Davis Mwamunyange na ujumbe wake amewasili jijini New York siku ya  Jumatano tayari kuhudhuria na kushiriki mkutano huo ambao  utafunguliwa siku ya alhamisi  na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon .
 Kwa  mujibu wa Waandaji wa Mkutano huu ambao ni  Idara ya Operesheni za Ulinzi wa Amani  ya Umoja wa Mataifa, ( DPKO) wameeleza  kuwa Zaidi ya  Wakuu wa Majeshi  100  watashiriki mkutano huu ambao   ni  wa kwanza wa aina yake kuwakutanisha  Wakuu wa Majeshi ya Ulinzi kwa wakati mmoja.
     Wakuu wa  Majeshi ya Ulinzi wanatarajiwa  pamoja na mambo mengine,  kujadili na kubadilishana  mawazo juu ya umuhimu wa  operesheni za ulinzi wa Amani katika kukabiliana na matishio mbalimbali ya  kiulinzi na kiusalama  yanayoikabili dunia hivi sasa.
Vile vile wakuu  hao  watautumia mkutano huu ambao  hautakuwa wazi ( closed meeting)kuongeza uelewa na ufahamu juu ya mazingira ya uendeshaji wa operesheni za ulinzi wa Amani , na wanatarajiwa  kutoa  mchango wa mawazo yao juu ya namna  ya   kuboresha    utendaji na  ufanisi wa  operesheni za ulinzi wa Amani.
Katika  miaka 70 tangu kuanzishwa  kwa Umoja wa Mataifa,  jumla ya misheni 68 za ulinzi wa Amani zilianzishwa na mpya kabisa ikiwa ni ile iliyoanzishwa  ( 2014)katika Jamhuri ya Afrika ya Kati ( MINUSCA).
Jumla ya wanajeshi 93,000 na polisi 13,000 kutoka nchi 120 wanahudumu katika misheni 16 ambazo  ziko katika mabara manne.Ambako pia kuna raia 17,000 wanaotoa huduma mbalimbali  zikiwamo za misaada ya kibinadamu katika misheni hizo.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali  Davis Mwamunyange ameambatana na  Brigedia Jeneral MG Luwogo,  Brigedia Jenerali HS Kamunde,  Lt. Col GM Itang’are na Maj CA Ngh’abi

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages