Breaking News

Your Ad Spot

Apr 14, 2015

CHADEMA KUCHANGIWA NA SIMU ZA MKONONI

indexNa Mahmoud Ahmad,Arusha.
…………………………………………
Chama cha Demokrasia na Maendeleo Kanda ya Kaskazini kimezindua rasmi mpango wa kuchangia chama hicho kupitia simu za mkononi ili kukiwezesha chama hicho kushinda katika Uchaguzi mkuu wa taifa utakaofanyika Octoba mwaka huu.
 
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ofisi za mkoa za chama hicho ,Katibu wa Chadema kanda ya Kaskazini Amani Golugwa amesema kuwa michango itakayokusanywa na wanachama na wapenzi wa chama hicho itawawezesha  kufanya kampeni nchi nzima na kuikomboa nchi hii kwa kupata viongozi bora.
 
Golugwa alisema kuwa kutokana na watanzania wengi kuchoshwa na uongozi mbovu wa CCM wanahitaji kukichangia chama hicho ambacho ndicho tumaini la pekee kwa Watanzania la kuleta mabadiliko ya kweli.
 
“Hatutaki tushindwe kufanya kampeni kwasababu hatuna fedha hivyo tunawaomba wanachama na mashabiki wa chama hicho kukichangia chama hicho kupitia simu zao za mikononi kwa kupitia namba maalumu tutakayowapatia” Golugwa
 
Alisema kuwa mpango huo umeanza rasmi na unakubalika kwa mujibu wa sheria za usajili wa vyama vya siasa kuwa chama kitapata mapato yake kupitia michango mbali mbali kwa wanachama.
 
Katibu huyo wa Kanda ya Kaskazini Amani Golugwa amewataka polisi na vyombo vya  usalama  pamoja na tume ya uchaguzi kuhakikisha kuwa wanafanya kazi kwa misingi ya haki na ukweli hasa katika kipindi ambacho nchi inaelekea  kwenye uchaguzi ili kuepuka kuhatarisha amani.
 
“Tusifanye masihara na amani ,tunahitaji tume huru na yenye uadilifu itakayofanya kazi yake vizuri bila kuegemea upande wowote” Alisema Golugwa

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages