"BUSARA YA MADIBA NI FUNZO KWA WANAHARAKATI NA WANASIASA WETU".Historia haina uchoyo na mawazo
kwa kila mwanadamu aliyejitosa kutengeneza historia.NELSON MANDELA ni
miongoni mwa wanahistoria waliowahi kuijua na kuitengeneza historia ya
dunia na kuwastaajabisha magwiji wa kihistoria wa huko ughaibuni kama
akina Hegel,almond na wengine wengi.Madiba alikuwa ni mwanasiasa
aliyeamini kuwa haki itapatikana kwa njia ya amani kabisa(non
violence).Ili kuweza kutimiza ndoto zake za kuwakomboa watu wake,silaha
kubwa ilikuwa ni mikutano ya hadhara,machapisho mbalimbali ya magazeti
na majalida yaliyobeba dhana ya ukombozi lakini pia aliweza kutumia
nguvu kubwa ya kuviunganisha vyama vingine vya kisisa kuwa kitu kimoja
vyama kama PAC,ANC viliweza kuungana na kuwa na dhamira ya dhati ya
kuwakomboa wana waafrka ya kusini.Chachu ya ukombozi ilichochewa haswa
na azma ya kishetani ya makaburu baada ya kuigawa Afrika kusini kwa
namna ilivyo wapa ardhi bora kabisa ya kilimo takribani asilimia 87
walijimilikisha huku asilimia 13 ya udongo mkavu wakiachiwa
wamatumbi,wamanyema na wakwere lakini pia makaburu hawa walitenga risavu
kwa waafrika kwa kuwatangazia uhuru.Mambo haya yalileta msuguano mkubwa
miongoni mwa wazawa,ndipo katika miaka ya sitini Mandela aliunda jeshi
la vijana almaarufu UMKHOTO WE SIZWE(mkuki wa taifa). "The spear of
nation" Umkhoto we sizwe ni kazi ya wanaume na wanawake pamoja na watoto
kwa maelfu waliojitoa mhanga ili kudai nchi ya mababu zao.Hatimaye
ukombozi wa afrika kusini uliweza kupatikana pindi De klerk alipotangaza
kwamba atakuwa makamu wa raisi chini ya rais mweusi yaani
MANDELA.TUMEJIFUNZA NINI KWA MANDELA? Kwanza roho ya kutolipa
visasi,baada ya miaka ishirini na saba jela,kwa mtu aliyeteswa kwa muda
wote huo wengi walitarajia kuwa kilikuwa kipindi kigumu kwa makaburu
lakini aliushangaza ulimwengu kwa kuwasamehe kwa yale yote
waliyoyafanya.Huu ni moyo wa kipekee wanasiasa wetu yawapasa kuuiga PILI
Mandela aliendelea kuamini njia sahihi ya ukombozi ni AMANI.Hili ni
funzo kwa viongozi wetu kuwa hata Diplomasia ni bora kuliko maandamano
na vita.Ushauri kwa viongozi mbalimbali wa kisiasa,HAKI ni dhana pana na
inaweza kupatikana hata kwa AMANI kabisa bila vurugu,maandamano na
vitisho viongozi wenye hekma za kidiplomasia kama MANDELA wanatufaa sana
kwa mazingira ya sasa TATU Mandela hakuamini katika uchu wa madaraka
ndio maana aliongoza kwa miaka minne pekee kwa kutambua dhana ya
demokrasia ktk uongozi.USHAURI viongozi wetu ni lazma wajitambua nni
maana ya kuwa ktk uongozi,lakini mbaya zaidi wengine hudhani uongozi ni
kuongoza taasisi nyingi,huku unakuta kiongozi wa chama na pengine ni
kiongozi wa taasisi,Tujifunzeni kwa madiba NNE na mwisho Mandela
aliamini siasa ni jumla na mstakabali wa maisha ya mwanadamu,lakini leo
hii uongozi umepoteza maana yake halisi pindi mtu anapokuwa mtaalamu wa
uongo,nghiliba na propaganda chafu dhidi ya wengine hujulikana kama
wanaharakati. Kuelekea uchaguzi mkuu wa oktaba mwaka huu yatupasa kuwa
makini na wanaojiita wanaharakati wanaotumia uelewa mdogo wa wananchi
katika siasa,uchumi na dhana nzima ya maendeleo kupata madaraka pia
propaganda chafu ndio mitaji yao kisiasa.Tanzania yenye NEEMA tele
inawezekana tekeleza wajibu wako wakujiandikisha sasa ili uweze kufanya
maamuzi sahihi kwa ajili ya kizazi cha sasa na baadae kupiga kura ni
haki na wajibu wa kila Mtanzania mwenye sifa kwa mujibu wa katiba
Your Ad Spot
Apr 7, 2015
Home
Unlabelled
NELSON MANDELA "BUSARA YA MADIBA NI FUNZO KWA WANAHARAKATI NA WANASIASA WETU"
NELSON MANDELA "BUSARA YA MADIBA NI FUNZO KWA WANAHARAKATI NA WANASIASA WETU"
Share This
About khamisimussa77@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269