Kamanda wa jeshi la zimamoto mkoa
wa iringa akikabidhi mbuzi kwa kaimu mkuu wa kituo cha Sister Theresa,
Sister Sister Winfrida Mhongole katika makabidhiano yaliyofanyika
kituoni hapo,
Kamanda wa Zimamoto akiwa na mmoja wa watoto wanaolelewa na kituo hicho cha sister Theresa.
Mmoja wa Askari wa jeshi la Zimamoto Eshter Aidan akiwa na watoto wanaolelewa katika kituo cha sister Theresa.
………………………………………………..
NA DENIS MLOWE,IRINGA
JESHI la Zimamoto mkoani Iringa limesheherekea sikukuu ya
pasaka na watoto wanaoishi katika kituo cha kulea yatima cha Sister
Theresia kilichoko Tosamaganga mkoani Iringa kwa kuwapatia misaada
mbalimbali.
Akikabidhi msaada huo Kamanda wa
Jeshi la Zimamoto mkoa wa Iringa Inspekta Kennedy Komba alisema lengo
kubwa la jeshi hilo ni kuwa karibu zaidi na jamii katika kutoa misaada
ambayo itawasaidia yatima walioko katika vituo mbalimbali mkoani hapa.
Alisema yatima wanakabiliana na
mazingira magumu katika kupata mahitaji muhimu hasa chakula, afya na
malazi hivyo ni jukumu la kila mmoja kuweza kuwasaidia kuondokana na
hali ya utegemezi.
“Tumeamua kugawa msaada huu kwa
kuguswa na matatizo mbalimbali wanayokabiliana nao vituo vingi vya
kulelea watoto hapa nchini katika harakati zetu za kuhahikisha watoto
yatima wanapata mahitaji muhimu katika maisha yao ya kil siku huu ni
mwanzo tu wa jeshi la zimamoto katika kuwa karibu na jamii na hii
tunafanya kila mwaka kuweza kurudisha pia katika jamii kile ambacho
jeshi hilo linapata” alisema Komba
Alisema msaada uliotolewa wa
mchele kilo hamsini, mbuzi, mafuta ya kupikia, sabuni na kuwapatia kifaa
cha kuzimia moto (Fire extinguisher) baada ya kuwapa mafunzo ya jinsi
ya kutumia vyote vikiwa na jumla ya thamani ya shilingi laki 250,000.
Komba alisema jeshi la zimamoto
litakuwa likitoa msaada wa aina hiyo kila mara ili kujiweka karibu na
jamii kuweza kutambua shughuli wanazofanya na kuwataka wadau wengine
kuiga jeshi hilo katika kuwasaidia watoto yatima.
“Jamii ya Kitanzania yatakiwa
kuunga mkono tabia ya kuwasaidia watoto yatima na kuwaimiza kupenda
masomo yao na jamii kutowatumia kama watoto wa kazi za ndani na
kuwahudumia kwa kila jambo wanalofanya kuliko kutumia muda mwingi katika
matumizi ya anasa” alisema Komba
Kwa upande wake kaimu msimamizi wa kituo hicho Sister
Winfrida Mhongole alilishukuru jeshi la zimamoto kwa msaada huo na
kuwataka wadau wengine wawe na moyo wa kujitolea kwa watoto yatima
wanaolelewa katika vituo tofauti mkoani hapa.
Alisema kituo kina jumla ya watoto 280 ambao
mbali na hao watoto 72 wanaishi kituoni hapo na wengine wako katika
shule mbalimbali wakisoma zikiwemo za msingi na sekondari.
Alisema watoto hao wamepokelewa kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo ya Iringa, Mbeya, Njombe, Morogoro, Dar es Salaam na Morogoro.
“Mbali na mapato yatokanayo na shughuli za kilimo
tunazozifanya kama kituo, kituo hiki kinaendeshwa kwa michango ya
wahisani mbalimbali wa ndani na nje. Kwa kweli hatuna wafadhili wa
kudumu,” alisema na kuomba wahisani waendelee kujitokeza kuwasaidia.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269