Breaking News

Your Ad Spot

Apr 14, 2015

TRA KUTOA MAFUNZO YA UKUSANYAJI WA KODI KWA WASHIRIKI 150

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo akiwakaribisha wageni katika hafla ya ufunguzi wa Mafunzo ya ukusanyaji kodi kwa waajiriwa wapya Leo Jijini Dar es Salaam. 
Mkuu wa Chuo cha uongozi wa Kodi (ITA) Prof. Isaya Jairo akimkaribisha Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Mafunzo hayo na kuwataka washiriki kushiriki kikamilifu kwenye kipindi cha mafunzo ili waweze kuwa na mbinu thabiti za ukusanyaji kodi kwa maslahi ya Taifa.
Naibu Mkurugenzi kitengo cha Rasilimali Watu Bw. Victor Kimaro akiwaeleza washiriki wa Mafunzo namna mchakato ulivyofanyika na kuwataka kuthibitisha ubora wao katika kipindi chote cha mafunzo.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Rished BADE akiongea na washiriki wa Mafunzo ya ukusanyaji kodi na kuwataka kufanya kazi kama watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania na kutumia fursa hiyo kujiimarisha kiutendaji kabla ya kuanza kazi rasmi ya ukusanyaji kodi inayohitaji uadilifu na ueledi wa hali ya juu katika kuitekeleza, wakati wa hafla iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya washiriki wa Mafunzo hayo wakifuatilia hotuba zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa ufunguzi wa Mafunzo hayo. 
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Rished Bade (kulia) akikata utepe kwenye boksi lililokuwa na Mtaala utakaotumia katika mafunzo hayo wakati wa ufunguzi uliofanyika leo jijini Dar es Salaam kushoto ni Mkuu wa Chuo cha uongozi wa Kodi (ITA) Prof. Isaya Jairo. 
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Rished Bade (kulia) akionesha mtaala utakaotumika katika mafunzo ya washiriki 150 waliodahiliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kushoto ni Mkuu wa Chuo cha uongozi wa Kodi (ITA) Prof. Isaya Jairo. 
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Rished Bade (kulia) akionesha mtaala utakaotumika katika mafunzo ya washiriki 150 waliodahiliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wa pili kushoto ni Mkuu wa Chuo cha uongozi wa Kodi (ITA) Prof. Isaya Jairo. 
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Rished Bade(wa sita kutoka Kulia) na Mkuu wa Chuo cha uongozi wa Kodi Prof. Isaya Jairo (ITA) (wa Tano kutoka kushoto) wakiwa katika Picha ya Pamoja na washiriki wa Mafunzo hayo baada ya kuyazindua leo Jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Hassan Silayo-MAELEZO)

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages